Stori: Shakoor Jongo
Ni tamaa ya ngono au ni nini?
Hivyo ndivyo unavyoweza kujiuliza baada ya kubainika kwamba mastaa
watatu Bongo, Wema Isaac Sepetu, mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ na Aunt Ezekiel Grayson wanatajwa kwenye mchepuko hatari wa
kuzungukana kimalovee, Ijumaa lina kila sababu ya kukujuza.
Mastaa
watatu Bongo, Wema Isaac Sepetu, mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ na Aunt Ezekiel wakiwa katika picha ya pamoja.
KILA KUKICHA
Ishu hiyo imebumburuka baada ya hivi karibuni mastaa kutengeneza vichwa vya habari kila kukicha kuhusiana na mambo yao hayo.
AUNT NA MOZE IYOBO
Duru za kihabari zinaonesha
kwamba hivi karibuni mwigizaji Aunt, bila ya kupepesa macho huku akijua
dhahiri kuwa ni mke wa mtu, Sunday Demonte alifungua kinywa na kuapa
kuwa hawezi kuachana na mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’
ambaye ni densa wa Diamond.
Aunt alitamka maneno hayo akijua fika
kuwa Moze Iyobo ni mume wa mwanamke aitwaye Mwengy ambapo wanaishi
Mbagala jijini Dar, wakiwa wamejaliwa mtoto mmoja.Mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’ akiwa na ‘Diamond Platnumz’.
AUNT KIOO CHA JAMII?
“Dah! Natambua kuwa msanii
ni kioo cha jamii lakini si kwa Aunt, hana hadhi ya kuitwa kioo cha
jamii kutokana na tabia yake ya kuchepuka wakati ni mwanandoa,” alidai
mmoja wa watu wake wa karibu.
Mdau mwingine wa sanaa za nyumbani
aliyejitambulisha kwa jina la Said, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar,
alimshangaa Aunt kukiri hadharani kuwa ana uhusiano usiofaa na Moze
Iyobo ambaye ni shemeji wa Wema kwa Diamond na yeye (Aunt) ni shosti wa
Wema.
Alisema kwamba, kwa hadhi yake, Aunt hakupaswa kutoa kauli hiyo ili
watu waendelee na minong’ono kuhusiana na yeye (Aunt) tofauti na
alivyofunguka bila aibu ukizingatia ni mke wa mtu.
“Unajua kwa nini
nasema Aunt anajidhalilisha au anawadhalilisha wanawake wenzake ni pale
anapokiri kuwa ndoa yake ipo tena bado anampenda mumewe huku anakuja
kusema kuwa anampenda Moze Iyobo, huo kama siyo mchepuko ni nini?”
alihoji Said.‘Moze Iyobo’ akiwa na familia yake.
WEMA NA DIAMOND
Uchunguzi ulionesha kwamba, huku
wakijua kila kitu waliwaruhusu Ahmed Hashim ‘Petit Man’ (Toto ya Wema)
na Esma Platnumz ‘kuchepuka’ huku Petit akiwa ni shemeji wa Diamond kwa
Wema.
Pia Diamond alifanya ‘misteki’ kumuacha mdogo wake, Esma ‘kuruka’ na Petit kwa kuwa ni shemeji yake.
KAJALA ANAINGIAJE?
Ilibainika pia kwamba Petit
aliwahi kuchepuka na mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’ ambaye ni mke wa
mtu, Faraji Agostino aliyeko gerezani na hilo likiwa wazi hata kwa hao
akina Wema na Diamond.
“Hebu jaribu kuangalia huo mzunguko na
mkanganyiko uliopo hapo. Yaani ni aibu tosha,” alisema mdau mwingine
kuhusiana na ishu hiyo.'Petit Man' akipozi kimahaba na Kajala Masanja, 'K'.
STEVE NYERERE AANIKA AIBU YAO
Hivi karibuni
kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar, Mwenyekiti wa Klabu ya
Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ aliwavaa mastaa hao
na kuanika aibu yao huku akimshutumu Aunt ambaye alifika maeneo hayo
akiwa ameongozana na mpenzi wake huyo wa sasa, Moze Iyobo.
Steve
alisikika akimwambia Aunt kuwa hamtendei haki Moze Iyobo na anamnyima
uhuru mkubwa kutokana na umri wake ambao anaweza hata kumzaa.
“Unajua wewe Aunt unastahili kuwa na mtoto mkubwa mwenye umri
usiokuwa tofauti na huyu Moze Iyobo.“Hivi kwa nini unajidhalilisha kiasi
hicho kwani wazee wenzako hujawaona hadi kumbemenda mtoto wa watu?”
alisika Steve akimpasha Aunt kwa sauti ya juu.'Petit Man' yule yule akiwa na dada yake 'Diamond Platinum', Esma.
NI SHARTI LA DIAMOND KWA WEMA
Akiendelea
kumpasha Aunt, jamaa huyo alikwenda mbali zaidi pale alipomwambia Aunt
kwamba anahisi kuwa uhusiano wake na Moze Iyobo ni sharti kutoka kwa
Diamond kumpa Wema ili alifanyie kazi na kumwambia kuwa ahakikishe yeye
(Aunt) anakuwa na Moze na Petit Man amuoe Esma.
“Unajua hivi karibuni baada ya Diamond kuandika yale maneno katika
Mtandao wa Instagram, nilisikia waliachana sasa naona Diamond
alimwambia Wema kama unataka nikurudie ahakikishe kuwa wewe Aunt unakuwa
na huyu mtoto (Moze Iyobo) halafu yule dogo mwenye rasta sijui mnamuita
Petit Man ahakikishe anamuoa Esma dada yake Diamond,” alisema Steve.Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ akifafanua jambo.
AUNT AWA MBOGO
Baada ya Steve kutoa dukuduku
lake mwigizaji huyo aligeuka mbogo na kumwambia Steve kuwa amuache kwa
raha zake kwani anampenda Moze Iyobo hata aseme nini hawezi kumuacha.
“Hata uongee nini Steve, siwezi kumuacha mpenzi wangu, nampenda sana na
hayo masharti unayoyasema kuwa ameyatoa Diamond unayajua wewe, niachie
nile raha zangu na Moze wangu,” alisema Aunt akimwangushia Moze Iyobo
bonge la ‘kisi’.
KUTOKA IJUMAA
Ni kweli wasanii ni kioo cha jamii
lakini kwa kuwa wamekuwa ‘vichwa ngumu’ kutenda yale yanayowafanya kuwa
vioo vya jamii ni vema jamii yenyewe ikachuja mema na kuyachukua kisha
kuwaacha wabaki na hayo machafu yao.
No comments:
Post a Comment