Na John Gagarini, Kibaha
WATU
wawili wamefariki dunia na wengine watano wamejeruhiwa baada ya magari
mawili likiwemo basi dogo la abiria waliyokuwa wakisafiria kugongana uso
kwa uso.
Kamanda
Mwambalaswa alisema kuwa ajali hiyo ilitokea Septemba 17 mwaka huu
majira ya saa 12:15 alfajiri maeneo ya Ubena Senge katika barabara ya
Morogoro.
Alisema
kuwa basi hilo dogo la abiria lenye namba za usajili namba T 663 BKP
lilikuwa likiendeshwa na Ally Abdul (34) lilikuwa na abiria wapatao 20
liligongana na lori hilo la mafuta aina ya Leyland Daf lenye namba za
usajili T 858 CLK na tela namba T 421 CKY mali ya kampuni ya Ramader ya
Jijini Dar es Salaam lilikuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Rashid.
Aliwataja
waliokufa kwenye ajali hiyo kuwa ni Neema Mile (39) na Jane Mtani (38)
ambao miili yao pamoja na majeruhi wako kwenye hospitali ya Rufaa ya
mkoa wa Pwani Tumbi kwa ajili ya matibab u na kusubiri ndugu wa
marehemu.
Aidha
alisema kuwa chanzo cha ajaili hiyo dereva wa basi hilo la abiria kuhama
upande wake kutokana na uchovu na usingizi unaotokana na kuendesha gari
usiku kucha bila kupumzika na inamshikilia kuhusiana na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment