Dar es Salaam. Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amesema
iwapo misingi ya uchaguzi ndani ya CCM italalia kwenye rushwa,
hataendelea kuwa mwanachama na kuonya kuwa tatizo hilo limefikia pabaya
na litakiangusha chama hicho.
Sumaye, ambaye alipewa adhabu ya kudhibitiwa kwa
miezi 12 kwa kosa la kuanza kampeni za urais mapema, alisema msimamo
wake wa kupinga rushwa na tabia yake ya kujishirikisha kwenye mambo ya
kijamii vinaweza kuwa sababu ya kutuhumiwa kufanya kampeni na baadaye
kupata adhabu hiyo.
Alionya kuwa vurugu zinazotokea sasa, hasa kwenye mikoa ya
Kusini si ajali, bali hasira za wananchi dhidi ya viongozi wao ambao
alisema wamejitenga baada ya kupata madaraka na hivyo wananchi wanatumia
kila nafasi wanayoipata kuwaadhibu.
Katika mahojiano maalumu na waandishi wa gazeti
hili, Sumaye ambaye alijitokeza kwenye kinyang’anyiro cha urais mwaka
2005 lakini hakupitishwa na CCM, alisema hawezi kuendelea kuwamo kwenye
chama endapo kitachagua viongozi kwa rushwa.
“Suala si kama mimi nagombea au sigombei… Hata
kama sigombei. Kama nitajiridhisha mwenyewe kuwa huyu amefika pale
(amechaguliwa) kwa sababu ya rushwa, sitakuwapo sehemu hiyo (kwenye
chama hicho), hata kama sigombei,” alisema Sumaye katika mahojiano hayo
yaliyofanyika nyumbani kwake Kiluvya, takribani kilomita 30 kutoka
jijini Dar es Salaam.
Sumaye, ambaye ndiye waziri mkuu pekee aliyemaliza
awamu mbili za jumla ya miaka 10 bila ya kuondolewa, alikuwa akijibu
maswali kuhusu mustakabali wake ndani ya CCM ambayo anadai imetawaliwa
na rushwa. Maswali hayo na majibu yake yalikuwa:
Waandishi: Mwanzo ulisema rushwa inapokithiri kuna
watu wanaweza wakatoka kwenye chama. Inavyoonekana katika mazungumzo
yetu haya, wewe ni mtu ambaye unaichukia sana rushwa. Unafikiri, hivi
(rushwa) inavyoendelea na labda kwenye uchaguzi wa mwakani itakuwa
hivyo, unaweza siku moja ukatoka CCM?
Sumaye: Hilo nafikiri nilishawahi kulisema…
nilisema kama misingi ya uchaguzi kwenye Chama Cha Mapinduzi italalia
kwenye rushwa, mimi sitakuwa sehemu ya hiyo. Hilo nilishalisema na wala
sibahatishi. Sasa suala si kama mimi nagombea au sigombei, hata kama
sigombei. Lakini… kama nitajiridhisha mwenyewe kuwa huyu amefika pale
(amechaguliwa) kwa sababu ya rushwa, sitakuwapo sehemu hiyo. Hata kama
sigombei.
Waandishi: Utakuwa radhi kusema sipo mahali hapa?
Sumaye: Sasa kama naweza kusema sasa, unataka nisemeje? niandike kwa damu? (anacheka).
Sumaye, ambaye alishindwa kwenye uchaguzi wa
wajumbe wa Nec mwaka 2012 kwenye Wilaya yake ya Hanan’g, alisema nchi
imefika mahali pabaya kiasi kwamba watu wanaona wakati wa uchaguzi ndiyo
halali kwao kupokea rushwa.
“Unajua, imefika mahali watu hawawezi kujitokeza
kwa sababu inaonekana mazingira yanayotakiwa ni ya rushwa. Kwa hiyo
anasema ah, ya nini? Hata usiende kwenye ngazi ya urais, hivi unadhani
hakuna watu wazuri ambao wangekuwa wabunge? Wako,” alisema mbunge huyo
wa zamani wa Hanang na kuongeza:
No comments:
Post a Comment