Dodoma. Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kuwa
siyo jambo baya kwake kutajwa kutaka kuwania urais katika uchaguzi mkuu
ujao 2015 na kwamba kujitokeza pia ni jambo jema.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti
hili nyumbani kwake mjini Dodoma juzi, ambapo alizungumzia mambo
mbalimbali, Pinda alisema kuwa jambo la msingi kwa wote wenye nia ya
kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi nchini ni kutambua kuwa urais ni
dhamana kutoka kwa wananchi na haupatikani kwa uamuzi wa anayegombea,
bali taratibu za vyama na wananchi watakaopiga kura.
Pinda maarufu kama Mtoto wa Mkulima alisema pia kwamba ni muhimu kwa watu wanaotaka kuwania urais wasikiuke misingi ya haki kwa kuingilia mchakato na kuwadhoofisha watu wenye mamlaka ya kuchagua mgombea urais, bali waachwe ili wafanye uamuzi wa haki kwa manufaa ya taifa, huku akisisitiza kufuatwa kwa taratibu za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Pinda maarufu kama Mtoto wa Mkulima alisema pia kwamba ni muhimu kwa watu wanaotaka kuwania urais wasikiuke misingi ya haki kwa kuingilia mchakato na kuwadhoofisha watu wenye mamlaka ya kuchagua mgombea urais, bali waachwe ili wafanye uamuzi wa haki kwa manufaa ya taifa, huku akisisitiza kufuatwa kwa taratibu za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Kujitokeza ni jambo jema, kutajwatajwa nako pia
ni jambo jema tu kwa maoni yangu. Ninachoweza kusema kikubwa, wote
wanaotaka kwenda kwenye hiyo nafasi, rai yangu kubwa ni moja tu,
watambue wanachotaka kwenda kufanya ni dhamana. Ni nafasi kubwa, lakini
ni dhamana tu unapewa kwa niaba ya Watanzania wengine wote.
“Kwa hiyo basi, uamuzi wa nani atakuwa, hauwezi
kuwa wa kwako wewe. Lazima tuuache mikononi mwa wale ambao kikatiba,
kisheria na kadhalika, ndiyo wamepewa hilo jukumu. La msingi hapa sisi
ambao tunataka kuingia kwenye dimba hilo, tuhakikishe hatuwadhoofishi
katika kufanya uamuzi wao wa haki kwa vishawishi, kwa vivutio, tuache
wafanye uamuzi kwa imani kwamba wanayemchagua atatufikisha pale ambapo
tunataka,” alisema Pinda.
Alifafanua: “Mimi sisomi sana mtandao, lakini
wakati mwingine nalazimika kusoma, kwa msingi huo hakuna haja ya
kurushiana maneno au kuchukiana kwa wanaotaka kugombea, kwani kati yao,
hakuna mwenye uhakika wa nani atakuwa. Kila mmoja anasema nami nijaribu,
unakwenda huko na moyo mweupe, kimtazamo ambapo unafanya kazi kihalali,
kwa haki, kiuadilifu, lakini mwishowe tujue kwamba uamuzi unabaki kwa
watu waliopewa dhamana ya kuteua mgombea katika hatua ya mwisho.
Tukiwapa fursa hiyo, naamini tutapata kiongozi mzuri.”
Hivi karibuni vyombo vya habari viliandika habari
zilizodai kuwa Waziri Mkuu Pinda alitangaza nia ya kuwania urais katika
Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015, akiwa mkoani Mwanza. Wengine waliotangaza
nia ya kuwania urais kupitia CCM ni January Makamba, ambaye ni Naibu
Waziri wa Sayansi na Teknolojia, na Mbunge wa Nzega, Dk Hamisi
Kigwangalla.
Wengine wanaotajwa katika mbio hizo ni pamoja na
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, Samuel Sitta (Spika wa Bunge
Maalumu la Katiba), Waziri wa Sheria na Katiba, Asha Rose- Migiro,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Steven Wassira,
Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri
Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini,
William Ngeleja.
Wingi wa wagombea
Akizungumzia wingi wa wanaojitokeza kutaka nafasi
hiyo ya juu ya uongozi wa taifa kupitia CCM, Waziri Mkuu Pinda alisema
kuwa siyo jambo baya akisisitiza kwamba jambo muhimu ni kuachia wenye
dhamana ya kuchagua mgombea, lakini akasema tatizo linaweza kutokea
iwapo makundi hayo yatagombana.
Alisema kwamba katika CCM siyo jambo gumu
kurudisha pamoja makundi tofauti ya waliowania nafasi ya kuteuliwa baada
ya mmojawao kuteuliwa na chama kukiwakilisha katika uchaguzi mkuu, huku
akisisitiza kuwa kama makundi yatagombana na kutukanana ndipo ugumu
hutokea.
No comments:
Post a Comment