KATIKA hali
ambayo siyo ya kawaida iliyowashangaza wakazi wa eneo la Ukonga
Mazizini kwa Makobe, baba mmoja aliyefahamika kwa jina la Elisha Zakari
amedaiwa kumpiga mwanaye wa kumzaa kipigo kama cha ng’ombe machungani na kusababisha azimie na kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Mtoto
huyo aliyepigwa ni Amani Elisha (10) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya
Msingi Maarifa iliyoko Ukonga, Dar es Salaam, baada ya kipigo alizimia
siku mbili. Tukio
hilo la kikatili lilitokea usiku wa Ijumaa iliyopita na sababu ya mtoto
huyo kupewa kipigo inadaiwa ni kutokana na utoro shuleni na kwamba hata
akienda
huwa haandiki.Waandishi wetu waliponasa tukio walimtafuta mama mzazi wa
mwanafunzi huyo maarufu kama mama Amani na mahojiano yakawa hivi:
Mwandishi: Mama ni kweli kuwa mume wako alimpiga mtoto wenu?
Mama Amani: Ni kweli baba yake Amani ndiye aliyempiga.
Mwandishi: Kwani huyu ni baba yake mzazi?
Mama Amani: Ni baba yake mzazi kweli, wakumzaa.
Mwandishi: Wakati mtoto anapigwa wewe ulikuwepo?
Mama Amani: Hapana,
sikuwepo nyumbani, nilikuwa kwenye shughuli zangu, niliporudi nikakuta
haya. Niliambiwa na majirani kuwa Amani kapigwa na baba yake. Hakukuwa
na jinsi, tulimpeleka mtoto hospitali kutibiwa baada ya kuzimia.
No comments:
Post a Comment