Mahakama nchini Misri imemhukumu kiongozi wa kidini wa kundi la Muslim
Brotherhood,Mohamed Badie kifungo cha maisha jela,yeye pamoja na wafuasi
wake wapatao kumi na wanne.
Badie amehukumiwa kufuatia kukutwa na hatia ya makosa ya mauaji na
ukatili na pia kutaka kumng'oa madarakani rais wa nchi hiyo Mohammed
Morsi mnamo mwaka 2013,Badie tayari ameanza kutumikia kifungo hicho .
Hata
hivyo mwanaharakati mashuhuri Alaa Abdel-Fattah yeye ameachiliwa huru
katika mahakama ingine,Alaa alihukumiwa miaka 15 jela kwa kushiriki
katika maandamano ambayo yalizuiliwa mnamo mwaka wa jana.
No comments:
Post a Comment