Li Na.
MCHEZAJI wa kwanza wa tenisi nchini China kushinda mashindano ya
Grand Slam, Li Na, amestaafu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya muda
mrefu.Li, mwenye umri wa miaka 32 ambaye ni staa namba 6 kwa mchezo huo duniani, alisema kuwa anaondoka katika mashindano ya tenisi kwa sababu ya majeraha ya muda mrefu, hasa kwenye magoti yake.
Alishinda Grand Slams mara mbili - Frenc Open mwaka 2011 na Australian Open mwaka huu.
Chama cha Tenisi nchini China kimepongeza juhudi zake za kuimarisha mchezo huo nchini mwake.
No comments:
Post a Comment