Nilishawahi kusema huko nyuma kwamba, mapenzi yanachukuwa sehemu kubwa
sana ya maisha yetu ya kila siku.Tunafanya kazi usiku na mchana lakini
pesa tunazopata tunazitumia kwenye kufurahia maisha na wapenzi wetu.
Ndiyo maana ukiwa hauko sawa kimapenzi, namaanisha ukiwa huna mpenzi
wakati unahitaji kuwa naye au unaye lakini anakukorofisha, hata mambo
mengine huwezi kuyafanya kwa ufasaha.
Lakini yule ambaye maisha
yake ya kimapenzi yako sawa, anapata anachokitaka kutoka kwa mpenzi
wake, utagundua anafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na furaha
haikauki.Wakati ukweli ukiwa hivyo, wapo ambao wanaachika kila siku kwa
sababu ya kushindwa kujua namna ya kuwashika wapenzi wao. Kuna ambao
kusalitiwa kumekuwa ni sehemu ya maisha yao kwa sababu hawajui yapi
wayafanye ili wapenzi wao wasifikirie kutoka nje ya uhusiano wao.
Kimsingi nimegundua wengi hatuna elimu ya kutosha juu ya mapenzi.
Unakuta mtu kaanzisha uhusiano na mtu ambaye yuko mbali lakini hajui
wanawezaje kulidumisha penzi lao. Mmeoana wote mnafanya kazi na ni
wanandoa, mnawezaje kuishi katika msingi sahihi? Hayo yote utayajua
endapo tu utajua sehemu sahihi ya kuweza kujifunza na kuwa na ufahamu
kuhusu mambo hayo.
Huenda wewe tangu umezaliwa hujawahi kujihusisha kimapenzi, leo
umeingia kwenye uhusiano na hujui chochote, kama huna elimu ya mapenzi
hata kama umzuri vipi, utaachika tu kama siyo kusalitiwa kila siku.
Ndiyo maana leo nimeleta mada hii ili kama ulikuwa hujui, uanze leo
kujiimarisha kwenye masuala ya mahaba. Kumbuka hapa nazungumzia mapenzi
ya kiutu uzima, yale ambayo huwezi kufundishwa shuleni, kusoma kwenye
magazeti, kuona kwenye vipindi vya kawaida vya televisheni au
kusikisiliza redioni.Mtandaoni
Mitandao imekuwa ni msaada sana katika
ulimwengu wa sasa. Hakuna ambalo utalihitaji usilipate kwenye mtandao.
Kwa maana hiyo basi, kama kuna jambo unataka kulijua kuhusu mapenzi,
kuwa rafiki wa mitandao husika.
Kwa mfano unataka kujua jinsi unavyoweza kumfurahisha mpenzi wako
mkiwa faragha. Ukiuliza mtandao, utakuletea.Licha ya kwamba lugha
unayotumika ni ya Kiingereza, naamini wengi wetu tunajua hata kama ni
cha kubangaiza. Ila zipo baadhi ya mada ukiandika kwa Kiswahili pia
unaweza kuzipata.
Majarida maalum
Yapo majarida yanayozungumzia
mapenzi kwa undani wake ambayo yanauzwa sehemu maalum kwa jili ya watu
wazima tu. Kama kweli wewe ni mtu mwenye uhitaji wa majarida hayo,
ukiulizia utayapata kwani huwezi kuyakuta yanauzwa kiholela.
Wakati mwingine yanauzwa bei kubwa lakini elimu utakayoipata ni kubwa
na huwezi hata kujutia fedha uliyotoa. Kwa mfano unanunua jarida la
shilingi 50,000 na ndani yake ukapata mada juu ya kuishi kwa furaha na
mpenzi wako, namna na kuidumisha ndoa yako, jinsi ya kumpagawisha mpenzi
wako muwapo faragha na kadhalika. Huoni itakuwa ni pesa ndogo
ukilinganisha na gharama ulizotumia kwenye harusi yenu?
Ongea na wataalam
Kuna wataalam wa mambo ya
mapenzi ambao wanaweza kukusaidia. Kwa mfano mimi nimekuwa nikitumia
muda wangu mwingi kushauri wasomaji wangu juu ya mambo yanayowakosesha
furaha katika maisha yao ya kimapenzi.
Siyo mimi tu, wapo wengi wakiwemo baadhi ya akina mama ambao wamekuwa
wakitumika sana kwenye kuwafunda wasichana kabla ya kuingia kwenye
ndoa.Kikubwa ni kujua watu sahihi wa kuwauliza mambo sahihi kuhusiana na
mapenzi. Nilichogundua mimi ni baadhi ya watu kuwa na aibu. Hivi
unaonaje aibu huku unataka kujua mambo nyeti ambayo unajua
kutokuyafahamu kunaweza kuihatarisha ndoa yako?
Angalia vipindi vya kikubwa
Kwa watu wenye uchu
na elimu hasa hii nyeti, inabidi wakati mwingine wakubali kuamka usiku
na kuangalia vipindi ambavyo vinazungumzia mapenzi kwa watu wazima.Mara
nyingi vipindi hivi huwezi kuviona mchana, wanaovirusha husubiri muda
ambao watoto wamelala. Ukiwa ni mpenzi wa kuvifuatilia vipindi hivi, ni
lazima utakuwa bora kwenye uhusiano wako.
Nunua CD
Huenda hata wewe una CD zako ambazo
mara nyingi unaziangalia usiku kabisa, ukiwa peke yako au na mwenza
wako. Hilo ni jambo zuri hasa linapokuja suala la kujiweka fiti
kimapenzi.
Katika hili naomba niseme tu kwamba, kuna ambao
wanazitumia CD hizi kujiharibu. Wanazinunua ili kujifunza mambo kadhaa
lakini mwisho wake wananogewa na kujikuta wakimaliza haja zao kwa
kuziangalia.
Niwaonye tu kwamba, ukizoea sana kuziangalia picha hizo ukiwa peke
yako kisha ukamaliza shida zako, unaweza kujikuta si mtu unayependa kuwa
na mpenzi tena. Wapo ambao leo hii hawataki kusikia kitu mpenzi, kisa
wakiangalia CD hizo humaliza haja zao! Ni sawa unaweza kumaliza haja
zako lakini madhara yake ni makubwa. Ndiyo maana nasema kwamba, tumia CD
hizo kujipatia ujuzi lakini si kumalizia haja zako.
Ni hayo tu ila kama unataka kujifunza zaidi kupitia mimi, usisite
kunitafuta. Kumbuka ujanja na ubunifu wako ndivyo vinaweza kudumisha
ndoa yako lakini ukiwa unaendesha maisha yako kibubusa, kaa mkao wa
kusalitiwa kama siyo kuachwa!
No comments:
Post a Comment