Na Gladness Mallya
MWANADADA
anayefanya vizuri kunako gemu la muziki Bongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’
hivi karibuni alinaswa akitoa meno yote nje baada ya kushuhudia sherehe
ya msanii mwenzake, Lucy Komba na kusema ya kwake hawezi kuizungumzia
kamwe.
Msanii mkongwe wa tasnia ya filamu bongo Ummy Wenslaus ‘Dokii’
Akizungumza na paparazi wetu, Dokii alisema amefurahi sana Lucy
kuolewa na Mzungu na alidhani kwamba ni mzee kama Waafrika wengine
wanavyopenda kuolewa na Wazungu wazee lakini amempata kijana mzuri
anayevutia hivyo ana bahati ya pekee lakini kwa upande wake ndoa hataki
hata kuisikia.
“Kuhusu mimi siwezi kuzungumzia na huwa sipendi kabisa kuzungumzia
suala la ndoa yangu kama nimeolewa au nitaolewa ila naendelea kumpongeza
Lucy kwani siyo msichana yule wa kujisikia wala nini anaongea na kila
mtu,” alisema Dokii ambaye hajawahi kumwanika mwanaume wake.
No comments:
Post a Comment