Deogratius Mongela na Chande Abdallah
DIWANI wa Kata ya Sinza kwa tiketi ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jijini Dar, Renatus Pamba ‘Mr. Simple’
anadaiwa kumshushia kipigo denti wa Chuo cha Ubaharia cha EMI jijini
Dar, Alpha Mohamed (18) mpaka kumsababishia kupoteza fahamu, Risasi
Jumamosi limenyetishiwa.
Kijana Alpha Mohamed anayedaiwa kujeruhiwa na diwani huyo.
Kwa mujibu wa mjomba wa Alpha, Aboubakar Ramadhan, tukio hilo
lilijiri Agosti 29, mwaka huu nyumbani kwa diwani huyo, Sinza-White Inn
ambapo chanzo cha kipigo hicho kikidaiwa kuwa ni denti huyo kukutwa
akipiga stori na binti wa diwani aliyejulikana kwa jina la Mage.
Naye Alpha mwenyewe akizungumzia tukio hilo kwa wanahabari wetu,
alisema siku hiyo usiku alipigiwa simu na Mage ya kumtaka wakutane ili
amjuze kilichojiri kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa rafiki yao
mmoja (hakutajwa jina) kwa kuwa Mage hakwenda kwenye shughuli hiyo.
Denti huyo aliendelea kuanika mambo kwamba, muda mchache baada ya
kukutana na Mage nje ya nyumba yao, alishangaa kumwona kijana mmoja
anatokea na kumwambia anaitwa na diwani huyo nyumbani kwake.Diwani Renatus Pamba ‘Mr. Simple’ anayedaiwa kumjeruhi kijana huyo.
“Mwanzoni nilisita wito huo lakini kwa vile sikuona kama nilikosea
chochote niliamua kwenda kwa diwani huyo lakini nikashangaa baada ya
kuingia tu, geti likafungwa na kuanza kupelekwa mzobemzobe mpaka
sebuleni.“Nilimkuta diwani pale sebuleni ambapo alianza kunishambulia
kwa kunipiga fimbo za fagio la njiti huku akisema natembea na Mage.
“Alinipiga kuanzia saa 6 usiku hadi saa 9 maeneo ya kichwani,
mgongoni na kifuani. Hali ilivyokuwa mbaya sana, alikwenda chumbani
kwake, nami nikajikaza na kupiga simu nyumbani, lakini akaja,
akazichukua simu zangu na kuzizima huku akisisitiza kwamba atanipiga
zaidi,” alisema Alpha.
Mjomba wa Alpha yeye anasema baada ya kupokea simu ya anko wake huyo,
hakujua alikuwa katika nyumba gani zaidi ya kumsikia akiomba msaada,
hivyo walianza kumtafuta bila mafanikio kwa kuwa simu zake zote zilikuwa
hazipo hewani.Kijana Alpha Mohamed akionyesha jeraha alilopata kutokana na kipigo kutoka kwa diwani huyo.
“Tulimtafuta sana huku tukimpigia simu mara kwa mara. Ilipofika saa 9
usiku sasa, kuna mtu akatutonya kwamba, Alpha alionekana akiingia kwa
diwani huyo.
“Tulikwenda kwa diwani, tukamkuta Alpha hajitambui hata kidogo. Mwili
ulikuwa umevimba, hasa sehemu za kichwani huku mguu wake mmoja
umeteguka.“Tulimchukua Alpha na kumpeleka Kituo cha Polisi Kijitonyama
‘Mabatini’ jijini Dar ambapo alipewa PF 3 kwa ajili ya kwenda kupata
matibabu, tulimpeleka Hospitali ya Palestina (Sinza).
“Pale, madaktari walitwambia Alpha ameathirika zaidi ndani kwa ndani
hasa sehemu za kifuani na mgongoni,” alisema mjomba huyo.Naye mama mzazi
wa Alpha, Zanura Ramadhan alisema familia imefungua jalada la kesi
lenye Kumbukumbu Na. KN/RB/7748/2014 SHAMBULIO na wamefanikiwa kumkamata
kijana ambaye alimw ingiza kwa diwani siku ya tukio.
Diwani huyo alipotafutwa kwa njia ya simu na gazeti hili na kusomewa
mashitaka yake, alisema na yeye amefungua mashitaka katika Kituo cha
Polisi Urafiki-Ubungo akimtuhumu Alpha kutaka kumbaka binti yake.
“Nikwambie tu, yule Alpha alikuwa na binti yangu Mage usiku na
alitaka kumbaka hivyo nimefungua mashitaka na amekamatwa,” alisema
diwani huyo.Alipoulizwa kuhusu madai ya kumpiga Alpha, alikana na kusema
hakumpiga yeye bali msaidizi wake wa nyumbani (yule aliyemtuma akamwite
Alpha).
No comments:
Post a Comment