welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday 8 October 2014

NEWS ALERT: MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR, OTHMAN MASOUD OTHMAN AFUTWA KAZI


Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman.
 
RAIS wa Serikali ya  Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali  Mohamed Shein, leo amemfuta kazi Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman  Masoud Othman na nafasi yake kuchukuliwa na Said Hassan Said.

Rais Shein  amefanya uteuzi huo wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 55 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984.

Mhe. Said  Hassan Said ameteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na uteuzi huo  umeaza rasmi leo 7, Oktoba 2014. Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Said Hassan  Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu.
Uteuzi wa  Mhe. Othman Masoud Othman umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53,54 (1)  na 55 (3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.

No comments: