welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday 8 October 2014

MAN U YATESWA NA MAJERUHI

Manchester United manager Louis van Gaal now sends half his players off for international dutyManchester United msimu huu imejaribu kujiimarisha katika idara ya ushambuliaji kwa kufanya usajili wa kuvunja rekodi nchini Uingereza wakiwa na nia ya kutaka kurejesha makali yao yaliyopotea msimu uliopita lakini uwepo wa majeruhi takribani tisa ndani ya kikosi cha mashetani wekundu hao kinaifanya klabu hiyo kuweweseka.


                                             

 Paddy McNair is Manchester United's fifth defender currently sidelined through injury
Hivi karibuni klabu hiyo imetokea kumuamini mlinzi kinda Paddy McNair aliyekuwa akishirikiana vyema na Muajentina Marcos Rojo katika kuimalisha ulinzi wa katikati wa klabu hiyo lakini katika kile kinachoonekana kama kuandamwa na jinamizi la mkosi wa majeruhi kijana huyu naye amelipotiwa kupata maumivu ya misuli daraja la tatu aliyoyapata siku ya Jumapili wakati timu yake ya Manchester United ilipokipiga dhidi ya Everton na kupata ushindi wa magoli 2:1.

Kuumia kwa McNair kunatimiza idadi ya walinzi watano wa wa klabu ya Manchester United wanaokaa nje ya uwanja kutokana na majeruhi ambapo wengine ni Luke Shaw (kifundo cha mguu), Jonny Evans (kifundo cha mguu), Phil Jones (misuli) na Chris Smalling (nyama za paja).
 Luke Shaw sits injured on the floor during Sunday's 2-1 win over Everton
Wachezaji Ander Herrera (mbavu), Jesse Lingard (kifundo cha mguu), Michael Carrick (mguu) na Ashley Young (nyonga) nao wanaungana na walinzi hao watano katika orodha ya majeruhi ndani ya United wakati Wayne Rooney anaendelea kutumikia adhabu yake ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo dhidi ya West Ham.
 Manchester United manager Louis van Gaal now sends half his players off for international duty

 Wakati Manchester United ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya majeruhi, Arsenal wao wanashika nafasi ya pili katika orodha hiyo na kibaya zaidi ni kuwa idadi kubwa ya wachezaji walio majeruhi kwenye kikosi cha Mfaransa Wenger ni wale wa kikosi cha kwanza. 
Mikel Arteta, Aaron Ramsey, Mathieu Debuchy, Olivier Giroud na Theo Walcott ni miongoni mwa wachezaji majeruhi wa klabu ya Arsenal na wengi wao ni wachezaji wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo. 
 Mathieu Debuchy was injured during the first-half of Arsenal 2-2 draw with Manchester City
 Ifuatayo ni orodha ta majeruhi katika vilabu mbali mbali vya EPL mpaka hivi leo:

ORODHA YA WACHEZAJI MAJERUHI KWA VILABU VYA PREMIER LEAGUE KWA MSIMU WA 2014/2015.

Manchester United -9
Arsenal- 7
Burnley -7
Everton -7
Newcastle -7
West Ham -7
Liverpool- 6
Southampton- 5
Chelsea -4
Stoke City- 4


Swansea City- 4 
Aston Villa- 3
Hull City -3
Sunderland- 3
West Brom -3
Crystal Palace- 2
Leicester City- 2
Manchester City -2
Queens Park Rangers- 2

No comments: