welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Monday, 13 October 2014

BALOZI WA FINLAND NCHINI BI. SINIKKA ANTILA AMTEMBELEA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimkaribisha Balozi wa Finland Nchini Bi. Sinikka Antila (kushoto) kabla ya kuanza kikao kilichojadili utekelezaji wa mradi mkubwa wa kuboresha umeme katikati ya jiji la Dar es Salaam. Pia kikao hicho kilihusisha ujumbe wa balozi wa Finland na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza na Balozi wa Finland Nchini Bi. Sinikka Antila na ujumbe wake pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Balozi wa Finland Nchini Bi. Sinikka Antila akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
Balozi wa Finland Nchini Bi. Sinikka Antila (kushoto) akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Finland Nchini Bi. Sinikka Antila (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo.

No comments: