BAADA ya
kuvuja kwa picha katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita,
iliyowaonesha askari wawili wa usalama barabarani wakiwa ‘kimahaba niue’
ndani ya sare za kazi na kusababisha kupoteza ajira zao kutokana na
kukiuka maadili, siri zaidi nzito zimezidi kuvuja kuhusiana na ishu hiyo
na Amani limemuibua afande wa kike baada ya kumsaka sana.
Askari
aliyefukuzwa kazi kutokana na kosa la ukiukaji wa maadili, Veronica
Mdeme. Kwa mujibu wa vyanzo makini kutoka wilayani Misenyi mkoani
Kagera, askari wa kike aliyeonekana kwenye picha hiyo chafu, WP. 8898
Veronica Mdeme, inadaiwa kuwa alipata uhamisho kutoka polisi mkoani humo
na kupelekwa katika wilaya mpya ya Misenyi mwaka 2011 ambako mwaka
mmoja baadaye, ndipo akapigwa picha hiyo iliyoleta gumzo kubwa ndani na
nje ya Bongo.
Ilidaiwa
kwamba, picha hiyo ilipigwa katika barabara ya lami iendayo Mutukura,
umbali wa Kilomita 50 kutoka Misenyi na kwamba askari hao walikuwa
katika Kituo cha Polisi cha Kyaka.
Nguzo ya umeme inayoonekana nyuma yao, ni zile zinazopeleka umeme nchini Uganda kutoka Bwawa la Umeme la Mtera, Tanzania.
ILIKUWA PICHA YA KISHKAJI TU LAKINI…
Habari
zilidai kuwa, askari hao Veronica, F.7788 Mpaji Mwasumbi na PC Fadhil
Linga, walikuwa zamu moja na kwamba picha hiyo ilipigwa katika mazingira
ya kishkaji tu lakini baadaye ikaja kuzua balaa kubwa.
Ilisemekana
kwamba, Linga ndiye aliyewapiga picha wenzake ambao habari
zisizothibitishwa zilisema kuwa walikuwa na uhusiano wa kijamii.
Madai
yalizidi kutiririshwa kwamba baada ya kupigwa kwa picha hiyo, Linga
alibaki na nakala katika kamera yake kwa muda wa miezi kadhaa kabla ya
kugundua kuwa kumbe ilikuwa ni dili.
AWAGEUZIA KIBAO
Ilidaiwa
kwamba, katika hali isiyotarajiwa, Mpaji na Veronica hawakuamini masikio
yao baada ya Linga kuwaambia kwamba alihitaji kupata ‘kitu kidogo’
kutoka kwao ili aweze kuendelea kuhifadhi siri ya picha hizo.
Ilisemekana kuwa afande huyo aliwaambia wawili hao kama ataivujisha picha hiyo kwenye mitandao ya kijamii, watapoteza kazi.
“Baada ya
kuambiwa hivyo, jamaa walilegea kabisa. Mwanzoni walitia ngumu lakini
walipoona jamaa amekomaa, hawakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana naye,
hivyo akawa anapata kitu kidogo kila alipojisikia na kuwa nipe nikupe
na hakuna uhakika kama dada Vero alisalimika kwenye mambo mengine kwani
naye alikuwa akitumia nguvu kubwa kuhakikisha mumewe hajui,” kilidai
chanzo hicho.
Veronica Mdeme akiwa kwenye pozi. WAAMUA KUJILIPUA, WAMSHTAKI
Ilielezwa
kwamba, baada ya ‘kutolewa upepo’ kwa muda mrefu na kuonekana kama
wangekuwa ATM ya kudumu ya Linga, Mpaji na Veronica waliamua kujilipua
na kwenda kumshtaki kwa kigogo wa juu wa jeshi la polisi mkoani humo
ambaye anatajwa kuujua mchezo mzima ulivyokuwa.
Ilisemekana
kwamba, kiongozi huyo alilichukulia jambo hilo kwa uzito wake na
kuwakalisha wote watatu ili kuzungumza nao.Iliendelea kudaiwa kuwa
katika kikao kati ya askari hao na bosi wao, wawili hao walikiri kupigwa
picha hiyo na kuomba msamaha, lakini wakamlalamikia mwenzao ambaye naye
alikiri kufanya kitendo hicho, kwa kuwageuza kuwa ATM.
Ilidaiwa
kuwa mkubwa huyo alimuamuru Linga kuzifuta picha hizo na kuwataka
kusameheana, kwani kitendo walichokifanya ni kibaya na kinachoweza
kuhatarisha ajira zao. Linga alikubali ‘kuzi-diliti’ picha hizo!
WAGAWANYWA, LINGA ARUDIA
Ikazidi
kudaiwa kuwa ili kuwafanya waishi kwa amani, waligawanywa katika vituo
tofauti vya kazi mkoani humo huku mmoja wao, Mpaji akipelekwa Dar ambako
alikwenda kusoma Chuo cha Polisi Kurasini.
“Wakiwa
katika vituo hivyo tofauti, Linga alitulia kwa muda mchache tu kabla ya
kuanza tena usumbufu wake, hasa kwa Veronica ambaye anadaiwa kuwa mke wa
mtu. Ni katika usumbufu huo wa mara ya pili, akina Mpaji wakaamua
kumjibu jeuri jamaa, hawakuwa na uoga tena kwa vile suala lao
lilishafahamika kwa wakubwa,” kilisema chanzo chetu.
Inaelezwa
kwamba majibu ya jeuri kutoka kwa Vero na Mpaji yalimuudhi Linga ambaye
kwa lengo la kuwakomoa, aliamua kuzitupa picha hizo katika mitandao
mbalimbali ya kijamii ambako nako zilizagaa kwa kasi ya moto wa kifuu na
kuwafikia watu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari
vilivyoamua kuripoti.
Veronica
Mdeme alipokuwa akidendeka na askari mwenzie. “Picha hiyo ilipoonekana
mtandaoni, moja kwa moja polisi walijua imewekwa na Linga kwa sababu
hakukuwa na mtu mwingine aliyefahamu kuhusu picha hiyo. Ndiyo maana wote
watatu walifukuzwa kazi siku moja, hawakuwa na sababu ya kuhangaika
kujua nani kaweka,” kilisema chanzo hicho.
PICHA YA MREMBO YAWA GUMZO
Baada ya
kufukuzwa kazi kwa wahusika hao watatu, kumekuwa na picha za mrembo
mkali ambaye amekuwa akifananishwa na Veronica huku kukiwa hakuna
uthibitisho wa moja kwa moja kama kweli ni yeye (angalia picha ukurasa
wa mbele).
Kwa
mujibu wa maoni lukuki katika mitandaoni, kama kweli mrembo huyo ndiye
huyo askari wa kike, basi jamaa aliyekuwa naye kimahaba, alistahili
adhabu yoyote kuliko kukosa mahaba hayo.
“Ni kama
walivyoimba wale watoto wa Yamoto Band, yaani nzi kufia kwenye kidonda
siyo ufala bali kupenda. Huyu mtoto mashalaah,” ilisomeka sehemu ya
maoni ya stori hiyo ambayo ndiyo habari ya mjini kwa sasa.
Juzi,
Amani lilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe ili
kumsikia nini kinaendelea baada ya askari hao kufukuzwa kazi lakini
hakuwa hewani.
Naye
msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Advera Senzo alipopigiwa simu na
kuulizwa alisema walishafukuzwa kazi hakuna kingine lakini akaelekeza
apigiwe simu Mwaibambe.
No comments:
Post a Comment