Mwezi, Wiki na Sasa siku zimebaki kwa ile Filamu Mpya na ya Kusisimua ya MAPENZI YA MUNGU
Kuingia Sokoni ambayo imewakutanisha wasanii mahiri wa hapa hapa
Tanzania ambapo Mmoja kati ya Wasanii waliocheza filamu hiyo Ni Msanii
wa Muziki wa Kizazi Kipya anayejulikana kama Linah Sanga, kwa
Kushirikiana na Elizabeth Michael bila Kumsahau Flora Mtegoha ambae ni
Mama Mzazi wa Marehemu Steven Kanumba watakuwa ndani ya filamu Mpya
iitwayo MAPENZI YA MUNGU...Ni Filamu ambayo Kisa chake na Mafunzo yake
yanasisimua lakini Pia ni Moja kati ya filamu ambayo kiukweli ina hadhi
na vigezo vya kimataifa......
Nimefika hapa leo sio kwa Ujanja wangu Bali ni Kwa "Mapenzi ya Mungu..."
Nimefika hapa leo sio kwa Ujanja wangu Bali ni Kwa "Mapenzi ya Mungu..."
Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" ni
moja ya filamu ambayo Msanii Linah pamoja na Mama Mzazi wa Marehemu
Kanumba wameonyesha uwezo wa hali ya juu na kuthibitisha kuwa kweli
Sanaa ni Kazi.
Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" itakuwa Sokoni Kuanzi Wiki hii Kwa Wauzaji wa Filamu kote Nchini.
Filamu hii itasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Ltd.
No comments:
Post a Comment