Mkuu
wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. Johm Mwakangale ambaye ndiye Mgeni Rasmi
katika Mkutano wa wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)
wanaoishi nyanda za Juu kusini waliowahi kusoma katika chuo hicho
kuanzia mwaka 1965-2014 na yeye akiwa ni mmoja wa wanafunzi ambaye
alisoma katika chuo hicho mwaka 1967 na ambaye pia alikuwa ni Mkufunzi
katika chuo hiki na Mlezi wa Umoja wa wana CBE waishio nyanda za juu
kusini akitoa hotuba yake ambapo, alikishukuru chuo cha CBE kwa kufanya
mkutano huu muhimu wa kuwaalika wahitimu wote kukutana pamoja pia
aliongeza kuwa CBE ni chuo cha Kuigwa kwa sababu hata Viongozi baadhi
yao Tanzania wamesoma katika Chuo hicho mfano Omar Kingi Mhasibu Mkuu wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Stagomena Tax Katibu Mtendaji
SADC, Harry Katillya aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Suzan Kaganda-RPC Tabora, Dkt. Ramadhani Dau Mkurugenzi
Mtendaji NSSF na Graciano Kanzugala Mwenyekiti wa TCCIA kanda za nyanda
za juu Kusini , Alimalizia kwa Kuzindua umoja huo wa wanafunzi na kusema
CBE ni chuo ambacho kimezalisha wataalam wengi . Mwisho alizindua Rasmi
Umoja wa wana CBE waishio nyanda za Juu kusini mkutano uliofanyika
Tarehe 4.10.2014
Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. John Mwakipesile akisaini kitabu cha wageni wakati akiingia katika Mkutano huo
Meza kuu
Muongozaji wa Mkutano MC Bwana Ben akiwa anatoa Muongozo wakati wa Mkutano huo
Mkuu
wa Chuo Cha Elimu ya Biashara Kampasi ya Mbeya Ndugu Deonise Lwanga
akitoa utambulisho pamoja na Kumkaribisha Mkuu wa Vyuo vyote vya CBE
Tanzania.
Mkuu
wa Vyuo vyote vya Elimu ya Biashara (CBE ) Profesa Emmanuel Mjema akitoa
nasaha zake na kueleza malengo makuu ya Mkutano huo, alieleza kuwa
wanafunzi waliowahi kusoma katika Chuo cha CBE kuwa ni Mabalozi wazuri
ambao ndio wanaweza kukitangaza vyema chuo hicho kwa kuwa wao ndio
wanajua vyema chuo hicho, aliongeza kuwa wanafunzi waliowahi kusoma
katika Chuo cha CBE wanasaidia chuo kwa kutoa mrejesho wa chuo hicho,pia
inasadia katika Elimu, na aliongeza kuwa Alumni ni muhimu katika
maswala ya kuandaa Semina, Makongamano na mambo kama hayo, Mwisho
Alimshukuru Mgeni Rasmi kwa kukubali mwaliko na kujumuika katika Mkutano
huo pamoja na wanachuo wote waliowahi kusoma katika chuo cha CBE
Makamu
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) , Mipango, Fredha na Utawala
Dkt. Peter Msami akitoa Salamu za Shukurani kwa niaba ya chuo cha CBE
Mkurugenzi wa Fedha wa Chuo cha CBE Bwana John Mwangobola akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa Mkutano huo.
Mwenyekiti
wa kwanza wa Umoja wa wana CBE waishio Nyanda za juu Kusini ambao
umezinduliwa Rasmi Tarehe 04.10.2014 Bwana Boyd Faustin Mwakyusa akitoa
neno la Shukurani Baada ya uteuzi huo
Msimamizi wa Taaluma kutoka Chuo cha CBE Kampasi ya Mbeya Bwana Kayombo akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo
Viongozi
wa kwanza wa Umoja wa wana CBE waishio nyanda za Juu Kusini wakiwa
pamoja na Mlezi wao Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. John Mwakipesile
wa nne Kutoka Kushoto Mara baada ya Uchaguzi huo
Washiriki wakiwa wanafuatilia Mkutano kwa umakini
Picha ya Pamoja
No comments:
Post a Comment