Alisimulia kuwa, katika kipindi hicho walikuwa kwenye mahaba niue
ambapo mara nyingi alikuwa akitoka kazini anamfuata nyumbani kwake
Mwananyamala, Dar.Aliendelea kufunguka kwamba alipomwambia tu kuwa ana
ujauzito wake ndipo mambo yalibadilika huku jamaa akitibuka utadhani
kamwagiwa pilipili iliyosagwa.
Grace akiongea jambo.“Ukweli mwazoni mapenzi yalikuwa shatashata lakini baada ya ujauzito, jamaa aliniruka futi mia.
“Mwanzoni alitaka nikatoe lakini nikakataa na kumwambia kwa nini niue
kiumbe kisicho na hatia ndipo akaingia mitini mpaka leo na ujauzito
una miezi sita. “Kila nikimwambia anasema siyo wake, ananitukana na
mwisho aliniambia kwamba nisubiri mtoto azaliwe ndiyo tukapime DNA
(vinasaba), sasa nateseka kuulea ujauzito peke yangu.“Naendelea kulea
hii mimba, najua Mungu atanisaidia, nitajifungua salama na mwanangu
nitamlea lakini inaniuma sana kutokana na majibu anayonipa na matusi ya
kila wakati.
BOND ANASEMAJE?
Ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilimsaka Bond na
kummwagia kila kitu ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Huyo dada mimi
simfahamu na ninaona wamepanga kunichafua yeye na Anti Lulu kwa sababu
nina meseji nyingi sana za huyo dada, nimewasiliana naye Facebook
akisema yupo naye hapo kazini kwake hivyo naomba mpotezee hizo habari
siyo za kweli.”
Gazeti hili lilifanikiwa kuziona meseji za Bond alizokuwa
akiwasiliana na Grace katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp ambazo
zilikuwa zimejaa matusi yasiyoandikika gazetini huku akimtaka mwanadada
huyo kusubiri ajifungue ndipo wakapime DNA ili kujua ukweli.
No comments:
Post a Comment