Idadi ya watoto wa
familia moja waliokufa kwa ajali ya moto katika nyumba ya wazazi wao
waliyokuwa wakiishi, mkoani Geita, imeongezeka kutoka watatu hadi wanne,
baada ya mmoja wao aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa
Bugando, mkoani Mwanza, kufariki dunia.
Mtoto huyo, Scolastika
(15), ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari
ya Mwatulole, alizikwa Septemba 14,2014.
Alisema alimwambia
mkewe, Angelina Gasper, wapige magoti na kuomba nusura ya Mungu baada ya
moto huo kuzuka katika nyumba wanayoishi.
Nyumba hiyo iliteketezwa usiku wa Septemba 7, mwaka huu, baada ya watu wasiofahamika kuimwagia mafuta ya petroli.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie.
Watoto
wengine waliotetekea katika ajali ya moto huo, ni Reginald Robert (9),
ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne na Sofia (6) wa Shule ya Msingi
Ukombozi na Remijius (4) wa Chekechea, walifariki papo hapo.
Mkewe, Angelina
akizungumza kwa shida kutokana na kuondokewa na watoto wake wanne,
alisema huo si msiba zaidi ya msiba, kutokana na kubakiwa na watoto
wawili kati ya sita, ambao wanne wakifariki katika tukio hilo.
Mganga Mfawidhi wa
Hospitali ya Wilaya, Dk. Adam Sijaona, alisema kuwapo kwa tukio hilo
kumemfanya akutane na mkasa, ambao hajawahi kukutana nao.
Afisa Mtendaji kata ya
Kalangalala, Hamad Hussein, alisema waliotenda tukio hilo walimimina
mafuta ya petroli milangoni na madirishani na kuilipua nyumba hiyo
iliyoezekwa kwa bati inawezekana kwa chuki binafsi ama migogoro ya
ardhi.
Mwenyekiti wa Serikali
ya Mtaa huo, Hassan Mcharo na Afisa Mtendaji wa Mtaa huo, Simfukwe
Ally, kwa pamoja wamelaani tukio hilo wakati wakizungumza na gazeti hili
juzi.
Mkuu wa Wilaya ya
Geita, Manzie Mangochie, akizungumza kwa masitikiko kuhusu tukio hilo,
alisema amesikitishwa na kitendo hicho na kuagiza kuhakikisha kuanzia
ngazi ya mtaa hadi wilaya wanashirikiana kuhakikisha waliohusika na
unyama huo wanakamatwa.
No comments:
Post a Comment