MWIGIZAJI kiwango enzi hizo Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ aliyepotea kwa muda, ameibukia
kwenye Runinga ya EATV na kumbutua staa wa mwenzake, Kajala Masanja
kwamba, anatumia nafasi ya kuonekana kwenye filamu kujipatia wanaume
kama si mabwana!Akizungumza kupitia Kipindi cha Mkasi kinachoratibiwa na Mtangazaji Salama Jabir, Jumatatu iliyopita, Nora alisema
fani ya uigizaji imevamiwa kwa sasa kwani kuna watu ambao wanaingia
kwenye gemu ili wauze sura na kuonekana na wanaume wapate ‘soko’
kiulaini.
Mwigizaji kiwango enzi hizo Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’.
Salama: “Mlela (Yusuf).”
Nora: “Huyo hamna kitu.”
Salama: “Steve Nyerere.”
Nora: “Huyo hamna kitu.”
Salama: “Hemed (Suleiman).”
Nora: “Hamna kitu hapo.”
Juzi tulimsaka Kajala
kwa njia ya simu hakupatikana, lakini mmoja wa watu wake wa karibu
alisema staa huyo ameshangaa sana Nora kutaka kurudi juu kwa kutumia
jina lake.
“Kajala amezima simu, lakini kamshangaa sana Nora, alishazimika, sasa anaonekana anataka kuwaka tena kwa kutumia jina lake,”
alisema mpambe huyo.
Aliongeza
kuwa, watu hao kupitia vitendo hivyo wamekuwa wakiichafua tasnia kiasi
cha wote kuonekana hawafai (samaki mmoja akioza, ni wote).
Nora alikwenda mbali
zaidi alipoulizwa na Salama ni nani na nani hawafai na nani wanafaa,
alishindwa kuwataja kwa majina moja kwa moja lakini mtangazaji huyo
akaomba ataje majina yeye kisha Nora aseme kama anafaa au hafai!
Salama: “Kajala.”
Nora: “Huyo hamna kitu.”
Salama: “Batuli.”
Nora: “Huyo pia hamna kitu.”
Salama: “Lulu.”
Nora: ”Huyo safi.”
No comments:
Post a Comment