Maofisa wa polisi wakiwa eneo ulipotokea mlipuko huo.
MAOFISA wawili wa polisi wameuawa katika mlipuko wa bomu uliotokea
leo kwenye wilaya ya Bulaq Abu-al-Ila jirani na Wizara ya Mambo ya Nje
jijini Cairo nchini Misri.
Mlipuko huo umetokea katika mtaa uliojaa watu wengi jirani na Mto
Nile na bomu hilo linadaiwa kutegwa chini ya mti uliokuwa katika eneo
hilo.
Mpaka sasa hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulio hilo.
Tangu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Mohammed
Morsi, Julai mwaka jana, Misri imekuwa ikishuhudia misururu ya milipuko
na mashambulizi yanayowalenga maafisa wa polisi na wanajeshi.
No comments:
Post a Comment