DIVA: ZITTO NI MUME WANGU.” Ikikolezwa na dondoo ‘Adai ni mke anayetambulika
kisheria’ na ‘Asema hayuko tayari kuachana naye kirahisi,’ ambayo
uongozi wa gazeti umekusudia kwa nia njema kutoa ukweli juu ya habari
hiyo.Ufafanuzi huu unalenga
kumaliza mkanganyiko uliojitokeza hasa baada ya kuwepo kwa madai kutoka
kwa mhusika ambaye ni Loveness Malinzi (Diva) kuwa, hakuzungumza na
gazeti kile kilichoandikwa na kwamba alikuwa anazushiwa; madai haya
aliyawasilisha chumba cha habari kwa njia ya simu na sehemu kuyaweka
kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Instagram.
Kama
hilo halitoshi, Diva alikana kuzungumza na mwandishi wa habari hiyo
ambapo alisema mazungumzo yao yalihusu mwaliko wa Kipindi cha Global TV Online ambacho kinarushwa na mtandao unaoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers inayomiliki pia Gazeti la Amani na si vinginevyo.
Malalamiko
haya ya Diva yalikuja muda mchache baada ya gazeti kutoka likiwa na
habari hiyo ambapo jopo la wahariri wa Amani kabla ya kuchapisha habari
hiyo walijiaminisha kuwa ni ya kweli kutokana na taarifa pamoja na
vielelezo vya rekodi ya sauti ya mazungumzo alivyoviwasilisha mwandishi
kwenye dawati kuthibitisha kuwa alifanya mazungumzo na mhusika kuhusiana
na msingi wa habari nzima iliyoandikwa.
Mheshimiwa Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Kama
tulivyoeleza, baada ya habari hiyo kutoka na kipande cha sauti
kuingizwa kwenye Tovuti ya Global Publishers, ndipo yalipoibuka madai
hayo huku baadhi
ya wasomaji wakieleza kuwa ile siyo sauti ya Diva; hapo ndipo uongozi
wa gazeti ulipoamua kufuatilia ukweli na kubaini yafuatayo.
Pamoja na ukweli kuwa
Mheshimiwa Zitto Kabwe (Mbunge wa Kigoma Kaskazini) na Diva wana
ukaribu, mazungumzo kati ya mwandishi na mwanadada huyo kuhusiana na
kauli yake ya: “Zitto ni Mume Wangu,” hayakufanyika na kwamba mwandishi
alipika habari na kutengeneza sauti ya Diva kwa lengo la kuwahadaa
wahariri kwa nia mbaya!
Kwa msingi huo sisi
kama chombo cha habari makini, kinachosimamia weledi, kulinda na
kuheshimu haki za binadamu; tunachukuwa nafasi hii kumuomba radhi Diva,
Mheshimiwa Zitto, sanjari na jamii kwa ujumla kwa usumbufu wowote
uliosababishwa na habari hiyo.
Aidha, uongozi
unapenda kuutangazia umma kuwa, hatua kali za kinidhamu zimeshachukuliwa
dhidi ya mwandishi husika sambamba na onyo kwa viongozi wote wa gazeti
kwa udhaifu uliojitokeza katika habari hiyo.
Tunaomba jamii ielewe
kwamba Global Publishers siku zote inasimamia UKWELI na kamwe hairuhusu
kabisa habari za uongo kuandikwa katika magazeti yake.
Jamii iendelee
kutuamini na kushirikiana nasi katika kusimamia weledi wa uandishi wa
habari. Milango ya kukosolewa iko wazi, hivyo kwa mwenye malalamiko
yoyote juu ya habari zetu, iwe ni uongo au kutotendewa haki, asisite
kuwasiliana na viongozi kwa hatua zaidi. Ndimi, Mhariri Kiongozi,
Magazeti Pendwa.
No comments:
Post a Comment