Filamu
zilizochaguliwa kuingia katika Tamasha hizo kutoka kampuni mahiri ya
utengenezaji na usambazaji wa filamu Tanzania ya Proin Promotions
Limited na ambazo zina ubora wa kimataifa huku filamu hizo kutoka Proin
Promotions ltd zikiiwakilisha vyema Tanzania.
Filamu
zilizoingia katika tamasha hilo na zenye ubora wa Kimataifa kutoka
Kampuni ya Proin Promotions Ltd ni pamoja na Kitendawili(feature),
Kigodoro(Feature), Sunshine(Feature), Network(Feature).
Filamu
hizi za Kitanzania zina sehemu moja tu yaani part 1 na sio Part 1 na
part 2. Kwa kuzingatia vigezo vya kimataifa vya filamu kuwa Na Sehemu
Moja tu yaani Part 1 ndio sababu filamu kutoka Proin Promotions
zimefanikiwa kupita mchujo ambapo Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambayo
haitaki part 1 na part 2 kwa lengo la kukuza tasnia ya filamu nchini.
Filamu
za Tanzania zenye part 1 na part 2 zimetupwa nje sababu waandaji na
wataalamu wa nje wameziona hazina ubora wa muda katika standard ya
kimataifa na vigezo vinginevyo.
Filamu
hizo za Tanzania zitaonyeshwa pamoja na filamu mbalimbali nyingine
zilizopita katika mchujo huo toka mataifa mabalimbali ikiwemo Canada,
Kenya, Uganda, Austalia, Rwanda, Spain, S.Africa, Guinea Bisau, Brazil,
Nigeria, Switzerland, Argentina, UK, Burundi, Morocco. Ili kuona List
nzima ya filamu hizo ingia hapa Selected Films Arusha Film Festival 2014.
Vilevile kutakuwa na zoezi la utoaji wa tuzo katika tamasha hilo la filamu kwa kazi nzuri.
No comments:
Post a Comment