Shirikisho la soka la Afrika CAF limeagiza klabu
ya Algeria Entente Setif kucheza mechi yake ya kufuzu kwa kombe la
mabingwa barani Afrika dhidi ya TP Mazemebe bila mashabiki .
Mechi hiyo imeratibiwa kuchezwa tarehe 20 Septemba Setif.Caf imefikia uamuzi huo kufuatia matukio kadha yanayokiuka mustakabli wa kandanda yaliyotekelezwa na mashabiki wa ES Setif.
CAF ilitumia ripoti za maafisa wake katika mechi zilizoshirikisha Setif katika hatua za mchujo lakini haikudokeza matukio haswa.
No comments:
Post a Comment