welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday 24 February 2016

Q Chillah kwenda kusaka soko la muziki Nigeria,atafanya kazi na nani?

q chillah
Msanii wa bongo fleva ,Q Chilla ameweka wazi kuwa siku za hivi karibuni atafunga safari kwenda Nigeria kufanya kazi zake za kimuziki ili kupanua soko.

Hata hivyo Msanii huyo amesema hajajua bado atafanya kazi na msanii gani wa Nigeria ila amejipanga kukabiliana na yeyote atayejitokeza kwani anaamini ni uwoga kupanga kufanya kazi na msanii fulani tuu.
kuna watuwengi ambao tunawasiliana nao kwa sasa,lakini nimeona niwafate kule kule Nigeria ilikuwa niende tarehe 20 lakini tumeongeza wiki mbili ili kuimarisha bendi kwanza ambayo nimeizindua..nimejiandaa kolabo na yeyote yule,kwa sababu ukisema fulani ina maana una hofu na watu fulani” alifunguka Q Chillah.

No comments: