welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Monday, 22 February 2016

Kumfukuza Dogo Janja ni kujitia hasara,tutampa adhabu tu – Madee

janjarooo
Rapper Madee bado haamini kama maneno aliyoyasema dogo Janja kuwa Tip Top Connection inambania yalitoka moyoni kwa msanii huyo kwa kuwa wakati sauti iliyovujishwa Janjaro akisema hayo jana yake wakikuwa wakimalizia video yake(ya dogo Janja).

Madee anaamini zilikuwa ni mbinu za Dogo janja kumpata msichana aliyekuwa akimtongoza kwenye mazungumzo hayo(Soma hapa).Hata hivyo Madee amesema hawawezi kutoa maamuzi yatakayoweza kumgandamiza msanii huyo licha ya kile alichokifanya kwa kuwa wameshatumia pesa nyingi kufanya nyimbo na videos kwa hiyo ratiba yake itaendelea japo atakuwa kwenye adhabu.
ratiba lazima ziendelee,tumeshaghalamika kwenye kufanya nyimbo na videos,ratiba yake iko pale pale japo Dogo Janja atakuwa chini ya adhabu” alifunguka Madee na kuongeza kuwa mwezi wa pili ndio mwezi wa Dogo Jaja kulingana na ratiba za Tip Top.
Source:AyoTv

No comments: