welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Thursday, 4 December 2014

MASTAA WAKUBWA WAMPIGIA SALUTI DIAMOND PLATINUMZ!

BAADA ya Jumamosi iliyopita msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kunyakua tuzo tatu kwenye tuzo za Channel O zijulikanazo kama Channel O Africa Music Video Awards 2014 (CHOAMVA), zilizofanyika Afrika Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita, mastaa mbalimbali nje na ndani ya nchi wamempigia saluti. 
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipozi . 
Diamond ambaye ameweka rekodi nchini kwa kuwa msanii pekee kuchukua tuzo tatu kwa mpigo huku tuzo hizo zikiwa ni pamoja na ya Mwanamuziki Bora wa Kiume Afrika Mashariki, Video Bora ya Muziki wa Afro Pop, Mwanamuziki Bora Anayechipukia hivyo alikosa tuzo moja tu ya Video Bora kwa mwaka. 
Msanii mkali kutoka Nigeria Davido aliyetoa pongezi kwa ‘Diamond Platnumz’. Katika makala haya tunakuletea baadhi ya mastaa waliompigia saluti Diamond na kumpongeza kwa hatua aliyofikia.SUNDAY MANGU ‘LINEX’“Ukweli nampongeza sana Diamond na kikubwa nasema ametisha sana na ametutoa kimasomaso.”
DAVIDO
“Tanzania imesimama! Diamond Platnumz ameweza tena!” aliandika mwanamuziki huyu wa Nigeria kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram. 
Msanii wa Hip hop Bongo, Madee akipozi. 
EMMANUEL ELIBARIKI ‘NAY WA MITEGO’
“Diamond anatakiwa kuwa muwazi kwa sisi wenzake ili tuweze kuleta tuzo nyingi Bongo. Atoe mianya kwa wasanii wenzake kwa kuwaonesha njia kwani Nigeria wasanii wake walifanikiwa kutokana na mmoja wao alipofanikiwa aliwaonesha njia ya kujipenyeza kimataifa zaidi.” 
Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’. LULU SEMAGONGO ‘AUNTY LULU’
“Kweli Diamond anastahili kwa sababu anajituma na anafanya vizuri, nampa hongera sana, aongeze bidii zaidi asibweteke kwa tuzo alizopata.”WAJE
“Waooh! Hongera mkaka kwa tuzo tatu.” Aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.
Msanii wa muziki kutoka Nigeria , Waje. MADEE ALI
“Diamond anastahili kwa kweli, wewe ni zawadi yetu, sasa hivi neno Bongo Fleva linatajwa Afrika nzima hakutakuwa tena na maswali mengi ukisema unatoka Tanzania, hongera sana.”
Katika kuwapa shukrani mashabiki wake kwa kumfanikisha kushinda tuzo hizo, Diamond atatinga nazo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar ambapo pia usiku huo atapiga shoo ya nguvu.


No comments: