welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Thursday, 4 December 2014

MASHABIKI WA DIVA WA ALA ZA ROHO WAMJIA JUU MENEJA WA CLOUDS FM!


Mashabiki wa kituo cha redio cha Clouds FM wiki hii wameungana na watu wengi mbalimbali kukipongeza kwa kutimiza miaka 15 tangu kianzishwe, lakini kuna kundi moja la watu halina furaha – mashabiki wa kipindi cha Ala za Roho kinachoendeshwa na Loveness aka Diva the Bawse. 
Kuna taarifa kuwa mtangazaji huyo mwenye mashabiki wengi, amesimamishwa kazi. Awali wasikilizaji wake waliambiwa kuwa Mrs GK, yupo likizo lakini baada ya kuona likizo ya mwezi mmoja inakuwa miezi, walianza kuhisi kuna kitu hakipo sawa. 
Kwa muda mrefu wamekuwa wakikitaka kituo hicho kuwapa majibu ya kwanini hawamsikii malkia wao bila kupata majibu. Wengine wamefikia hadi hatua ya kwenda kwenye kituo hicho kuuliza kunani na bado wanadai wahusika wamekuwa wakiwakwepa. 
Na sasa, mashambulizi yao wameyahamishia kwa meneja wa vipindi wa kituo hicho, Sebastian Maganga ambaye post yake ya juzi katika birthday ya Clouds FM iligeuka uwanja wao wa kumwaga malalamiko yao. 
“Brother @sebamaganga turudishiee #alazaroho na mrembo wetu @divathebawse tutaandamaanaa MZEE tujee mjengoniiii tumemis saut ya kumtoa nyoka pangonii please tunampenda @divathebawse yuko wapiii bnaaaah brother,” aliandika Young wa Leo.

No comments: