welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Sunday, 12 October 2014

SHEPU YANGU NI KAMA ANDAZI LILILONONA NDIO MAANA NAPATA WANAUME! DIDA WA TIMES FM ATOA SIRIMtangazaji wa kituo cha Redio Times, Hadija Shaibu ‘Dida’.Aliweka bayana kwamba anaachika na kupata mwanaume mpya haraka kwa sababu ana shepu ya kalimati (aina ya andazi linalonona).
MTANGAZAJI wa kituo cha Redio Times, Hadija Shaibu ‘Dida’, juzikati aliamua kutoa siri yake ya moyoni na kuweka wazi juu ya tabia yake ya kuachika na kupata mume mpya mara kwa mara.
Mtangazaji wa kituo cha Redio Times, Hadija Shaibu ‘Dida’ akipozi kwenye bethidei ya Rose Ndauka.“Naomba watu wajue kuwa ukoo wangu, Rose na wenzake wao Mungu aliwapatia shepu na urefu wa umbo lakini mimi nina shepu ya kalimati na ndiyo maana napata waume...ingawa kwa leo sina mume wala mchumba,” alisema Dida alipokuwa kwenye bethidei ya mwigizaji Rose Ndauka iliyofanyika juzikati katika Ukumbi wa Collesium, Kariakoo, Dar.

No comments: