welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Sunday, 12 October 2014

BAHATI BUKUKU ANADAIWA KULIZWA NA MUMEWE


Staa mkubwa wa Muziki wa Gospel Bongo, Bahati Lusako Bukuku anadaiwa kulizwa baada ya ‘rumansi’ kuenea kwamba mumewe, Daniel Basila ‘Dany’ anataka kuuza nyumba yao.Staa mkubwa wa Muziki wa Gospel Bongo, Bahati Lusako Bukuku.Habari kutoka kwa chanzo chetu makini, madai ya mumewe kutaka kuuza nyumba yao iliyopo Mbezi-Salasala jijini Dar, yaliibuka hivi karibuni huku Bahati akiwa hajui mchezo unaoendelea. 
Ilisemekana kwamba nyumba hiyo ilijengwa na wawili hao wakati wa uhai wa ndoa yao kabla ya kutengana miaka kadhaa iliyopita ambapo Bahati alimwachia Dany nyumba hiyo. 
Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, gazeti hili lilimtafuta Bahati ambaye alisema hajui chochote hivyo aulizwe mumewe. 
Jitihada za kumpata Dany hazikuzaa matunda kwani simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi (sms) hakujibu pamoja na kwamba ilionesha kupokelewa (delivered).

No comments: