welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Sunday, 12 October 2014

FLORA MVUNGI AFUNGUKA MAUHUSIANO YAKE NA DUDE

Tunamalizia makala haya tuliyoyaanza wiki iliyopita. Flora amefunguka mengi yahusuyo safari yake ya kisanaa!UHUSIANO NA DUDE
Mwandishi: Kuna tetesi kwamba ulikuwa na uhusiano na Dude na alitaka akuoe?
Flora: Dude namheshimu sana na mara nyingi alikuwa ananipenda kwa sababu nilikuwa mtiifu sana kwake naona ndiyo sababu ya watu kuzungumza maneno hayo. Sikuwahi kufikiria kuolewa na Dude au kuwa na uhusiano naye.WANAUME MAARUFU
Mwandishi: Je uliwahi kutoka na wanaume wangapi ambao ni maarufu?
Flora: Niliwahi kutoka na mmoja tu ambaye ni Boniface Amban lakini niliachana naye baada ya magazeti ya Global Publishers kufichua maovu yake.Mwandishi: Ni maovu gani hayo ambayo uliyagundua?
Flora: Niligundua kwamba Amban alikuwa na mke na watoto huko Kenya.

WALIVYOACHANA
Mwandishi: Vipi baada ya kuachana, hakukutafuta ili mmalize tofauti zenu?
Flora: Niliachana naye akiwa hukohuko Kenya nami nikiwa kambini nikahama kabisa nyumba ambayo nilikuwa nikiishi kwani alikuwa anapajua hata kwa wazazi alikuwa anapajua pia hivyo tukaenda kupanga chumba na Shilole (Zuwena Mohamed).

BIFU
Mwandishi: Kuna habari kwamba wewe na Shilole mna bifu kali, vipi kuhusu hili?
Flora: Siyo kweli, kabla ya kufunga ndoa tulimaliza tofauti zetu na roho yangu iko nyeupe kabisa.

WALIVYOKUTANA NA H. BABA
Mwandishi: Hebu tueleze ulianza vipi uhusiano na H. Baba mpaka sasa ni mumeo?
Flora: Wakati nikiwa na uhusiano na Amban nilikutana na H. Baba katika Viwanja vya Leaders Club akanitongoza lakini nikamkataa lakini nilikuja kukutana naye tena akaniambia kwamba ana muvi yake anataka kunishirikisha.

ENHE!
Mwandishi: Ulikubali kucheza hiyo muvi yake?
Flora: Nilimkubalia lakini nikawa nina muvi yangu ya kumalizia nikamwambia naye ashiriki yangu akakubali baada ya kumaliza ndiyo tunajiandaa kuanza ya kwake nikapata dharura na kushindwa kucheza ya kwake, alinikasirikia sana tukawa hata hatuongei.

WAPATANA
Mwandishi: Baada ya kuchuniana bila kuzungumza ilikuwaje mpaka mkaja kuwa vizuri na kuanzisha uhusiano?
Flora: Siku moja mimi na Shilole tulienda club Sun Cirro sasa wakati tunaingia tukamuona H. Baba na rafiki zake ndipo Shilole akanilazimisha tukamsalimie nikakataa lakini aliendelea kuning’ang’aniza ndiyo nikaamua kwenda kumsalimia.

PENGO LA AMBAN LAZIBWA
Mwandishi: Nini kiliendelea baada ya hapo?
Flora: Baada ya kumsalimia ndipo mawasiliano mazuri yalianza kwani kwa kipindi hicho sikuwa na mtu baada ya kuachana na Amban.

WALIPOANZA UPYA
Mwandishi: Mlianza uhusiano wa kimapenzi upya mwaka gani?
Flora: Uhusiano wa kimapenzi rasmi tulianza mwaka 2012 ambapo nilihama nilikokuwa nikiishi na Shilole nikahamia kwa H. Baba tukaishi kwa mwaka mmoja ndipo tukafunga ndoa.

MAJUNGU
Mwandishi: Kabla hamjafunga ndoa na H. Baba maneno yalikuwa mengi sana kuhusu ninyi, ulikuwa ukijisikiaje?
Flora: Kweli wasanii wenzetu waliongea maneno mengi sana lakini walikuja kukaa kimya baada ya kila kitu kwenda sawa yaani kuona tumefunga ndoa.

MAISHA YA NDOA
Mwandishi: Unayaonaje maisha ya ndoa?
Flora: Mazuri, tunapokuwa wawili imekuwa rahisi sana kusaidiana kwa hiyo mapendelezo yaliyo ndani ya akili zetu yanasaidia sana kudumu kwenye ndoa na maisha kuwa mazuri zaidi.

WIVU
Mwandishi: Kuna tetesi kwamba mumeo H. Baba ana wivu sana na hapendi utoke peke yako, ni kweli?
Flora: Mimi mwenyewe nina wivu sana lakini huwa naangalia na ninachokionea wivu, H. Baba hanibani kwa sababu tunaaminiana kwa hiyo ananiachia nikitaka kwenda popote ananiruhusu.

MUZIKI
Mwandishi: Ilikuwaje ukaingia kwenye muziki na nani aliyekushawishi?
Flora: Nilikuwa napenda muziki tangu nikiwa mtoto lakini nilikuwa sijapata pa kuanzia lakini tangu nimekuwa na H. Baba amekuwa akinisaidia mambo mbalimbali ya kimuziki ambayo yamenisaidia na kuniendeleza sana.

MTOTO
Mwandishi: Ulijisikiaje siku uliyompata mwanao Tanzanite?
Flora: Yaani nilifurahi sana na siwezi kusahau siku hiyo kwa kweli.

NDUMBA
Mwandishi: Kuna tetesi kuwa mnatumia ndumba sana kwenye sanaa, ni kweli?
Flora: Tangu nianze sanaa sijawahi kutumia ndumba na sijui hiyo kitu ikoje.

IDADI YA MUVI
Mwandishi: Mpaka sasa una muvi ngapi ambazo ni za kwako?
Flora: Nina muvi tano ambazo ni Bado niko Hai, Wema wa Mama wa Kambo, Mama Kijacho, Trafiki Pori, Bush Star Search.

No comments: