welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Friday, 12 September 2014

KAJALA, HIVI HUKUJIFUNZA KITU KWA WEMA?

KAMA mwandishi, sijawahi kukutana na Kajala Masanja na kufanya mazungumzo naye, lakini kama mdau nimeona kazi kadhaa za muigizaji huyu mwenye jina kubwa katika Bongo Movie.Anajitahidi kuigiza na katika uhalisia wake, huyu ni miongoni mwa wadada wanaoweza kuibeba tasnia hii na kuifikisha katika levo zingine za mbali na kuiletea sifa nchi yetu.
Nimewahi kusoma simulizi juu ya maisha yake, inasisimua sana, hasa alipokuwa akizungumzia sakata lililosababisha yeye na mumewe kukamatwa, kufikishwa mahakamani na hatimaye kuhukumiwa jela. Amepitia maisha yanayotosha kumpa mifano na mafunzo mengi ya maisha.
Kama siyo shoga yake Wema Sepetu kumlipia fedha za faini alipohukumiwa pale Kisutu mwaka mmoja uliopita, hivi sasa tungekuwa angalau tumeanza kumsahau Kajala, kama ilivyo kwa mume wake Agostino Faraji.
Lakini unapomuona maisha anayoishi hivi sasa, unashindwa kujizuia kujiuliza kama ana chochote cha kujifunza na kujutia katika maisha anayopitia, hasa katika matumizi ya fedha.Wanaomfahamu vizuri wanasema hivi sasa msichana huyu ana fedha za kutosha, kiasi cha kumfanya atembee akiwa na wapambe, si unajua tena kibongobongo?
Sijajua ni fedha kiasi gani, lakini unapomuona msichana kama Kajala, anakwenda kumtunza mtu burungutu la shilingi laki sita na ushee, ni lazima ukubali kuwa anazo za kutosha.
Enzi za ujana wetu, tulizoea kuwaona watu walioitwa Mapedeshee wakifanya madoido hayo katika kumbi za starehe na kwenye mikusanyiko. Na ninawakumbuka bado, akina Fikiri Madinda, Juma Banatoz ‘JB’, Papaa Msofe, Muzamil Katunzi, Papaa Chosta, Hussein Makabyureta, Rama Mutoto ya Ng’ombe, Jack Pemba ‘JP’ na wengineo wengi wa enzi zao.
Sitaki sana kuingia kwa undani kujua nini kimewasibu watu hawa kwa sasa, lakini ushahidi wa mazingira unaonyesha jamaa wamebadili staili ya maisha, bila shaka baada ya kugundua walikuwa wanapotea, kwa sababu walikuwa wanayanunua majina yao kwa bei kubwa sana.
Shoga yake Kajala, Wema Sepetu, miezi michache iliyopita naye alikuwa katika hali kama hiyo, akitapanya fedha kwa staili ya kutembea na wapambe wengi, huku akigharamia matumizi yao, hata yale yasiyo na msingi.
Simfundishi namna ya kutumia fedha zake, lakini ni ushauri tu ambao anaweza kuufuata au kuushiti. Pesa haitoshi. Anaweza kuziona nyingi leo, lakini sidhani kama zinaweza kufika kesho.
Katika kutengeneza maisha, kesho iko mbali sana, lakini kwenye matumizi, kesho ni kufumba na kufumbua tu.

Watu wenye fedha zao tunaowajua, hawana ujuha wa kumwaga hela ovyo kwa lengo la kujitangaza, badala yake kama kurudisha sehemu ya hela kwa jamii, hula na watoto yatima, wazee wasiojiweza na wakati mwingine kuwapa mahitaji muhimu kama vyakula na mavazi.
Kajala bado ni binti mdogo. Kuwa na shilingi milioni 50, 100 au bilioni moja siyo kufika, bali ni mwanzo mzuri wa kutengeneza maisha ya baadaye. Nimshauri awekeze katika kilimo, majengo au ufugaji, uwekezaji ambao baada ya miaka michache, fedha zitaanza kutiririka bila kikomo na hivyo kumpa uhakika angalau.
Hana sababu ya kujenga jina kwa sababu tayari analo ila ana ulazima wa kujenga maisha kwa vile hana. Sifa za kijinga ndiyo zinazowasumbua sana wasanii, wanashindwa kuyajenga maisha yao kwa pesa wanazozipata kutokana na fursa mbalimbali wanazokutana nazo.
Hela zinapokuja hazipigi hodi na uzuri wake zinapoondoka, mwenye kuzimiliki anajua kuwa zinaondoka. Kajala anamjua Bill Gates? Ni tajiri wa kutupwa, lakini kila siku anakuwa mtu wa kwanza kufika ofisini kwake, kuhakikisha utajiri wake hauyumbi.
Leo mdogo wangu Kajala umepata mkondo unautumia kutafuta sifa, badala ya kujijengea misingi imara ya maisha yako ya baadaye!


 

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  ADVERTISE HERE


Forum

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by kathy paramores Aug 28. 19 Replies
Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!
Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by anilahsan Jul 19. 79 Replies
Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KILA MARA, TATIZO NI NINI?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by navarrohart Jun 8. 37 Replies
VITENDO VYA KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KWA SASA VIMEZOELEKA. KATIKA NCHI MBALIMBALI WATANZANIA WAMEKUWA WAKIKAMATWA KWA UBEBAJI WA MADAWA HAYO. JE, TATIZO NI NINI? NA NINI KIFANYIKE?
Tags: MARA, TATIZO, NI, NINI?, KILA

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI NI KWAMBA LIMESHINDWA KAZI?

Started by GLOBAL in Maisha. Last reply by anilahsan Jun 26. 72 Replies
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Jeshi la Polisi…

SIMBA SC WAMTUPIA VIRAGO JUMA KASEJA

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Aicar Salewa May 23. 5 Replies
TIMU ya Simba SC leo imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake mahiri, Juma…

JE, NI SAHII KWA JESHI LA POLISI KULIPUA MABOMU WAKATI WANANCHI WAKIAGA MIILI YA WENZAO?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by anilahsan Jul 12. 21 Replies
Juzi (Jumanne) polisi walilipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wenzao watatu waliopoteza maisha katika…

UKIMYA WA VYOMBO VYA DOLA KUTOA TAARIFA ZA MATUKIO YA MAUAJI NA UTEKAJI NI ISHARA KUWA WANAHUSIKA?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by LUPILYA GREGORY SIMON Dec 19, 2013. 7 Replies
Absalom Kibanda akiwa ICU.USIKU wa Jumanne ya Machi 5 kuamkia Machi…
Tags: UTEKAJI, NA, MAUAJI, NI, ISHARA

KIPIGO CHA BAO 2-1 KWA MAN UTD, KOSA LA MWAMUZI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Joe reggan Sep 3. 11 Replies
JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!

No comments: