welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Monday 8 September 2014

AISHA BUI: SIKUVUNJA NDOA YA AMINA CHIFUPA!

WIKI iliyopita tuliwadondoshea staa wa sinema za Kibongo, Aisha Bui ambaye mlimbananisha na kwa maswali kibao ambayo wiki hii anayajibu.
UNGANA NAYE…

Staa wa sinema za Kibongo, Aisha Bui akipozi.
ANASUBIRI NINI KUOLEWA?
Dada Aisha nasikia hujaolewa, unasubiri nini, ona umri unasonga? Dismas, Lindi, 0782713879
AISHA BUI: Kuolewa ni uamuzi hivyo bado sijaamua.

KUHUSU MPAKANJIA
Aisha mimi nilitaka kujua ile miaka ya nyuma kuhusu wewe kutoka kimahaba na marehemu Meddy Mpakanjia hadi ukaharibu ndoa ya marehemu Amina Chifupa, hivi ilikuwa ya kweli au walikuzushia? Selemani Alifa, Dar, 0718803204

AISHA BUI: Sikuvunja ndoa ya Amina (Chifupa), Meddy alikuwa ni mpenzi wangu lakini hakunioa kwani mimi siyo wa kwanza mbona aliwahi kutoka na wasichana wengine pia.
MAFANIKIO
Aisha una muda gani tangu uingie kwenye tasnia ya uigizaji na umepata mafanikio gani? Amiri Salumu, Dar, 0653252416
AISHA BUI: Nilianza sanaa mwaka 2010 lakini haikuwa ile moja kwa moja, mafanikio bado sana kwani muda mwingi nilikuwa na safari za nje ya nchi ila kubwa ni kujulikana tu.

KUPOROMOKA
Aisha wewe ni msanii mahiri wa filamu Bongo, je, unazungumziaje kuporomoka kwa tasnia ya uigizaji wa filamu juu ya kazi zenu kuibiwa na wajanja wachache kila kukicha? Salim Liundi, Dar, 0659601205
AISHA BUI: Sisi tunauza filamu kwa wasambazaji lakini kwa Tanzania sheria haifanyi kazi katika kuzilinda kazi za filamu kama zilivyo nchi nyingine hivyo serikali inatakiwa kutuangalia upya.
ALIKATALIWA?
Aisha eti jamaa uliyezaa naye alitaka kukuoa lakini alikataliwa kwenu kwa sababu dini zenu tofauti?  Muddy Madiley, 0652672805
AISHA BUI: Mimi sijawahi kuwa na mwanaume mwenye dini tofauti na mimi na huyu niliyezaa naye ni Muislam kama mimi, bado hajafika kwetu.

ANATAKA KUMUOA
Aisha nipe nafasi nataka nikuoe, uzuri ulionao lazima uolewe. Muddy, 0755462633
AISHA BUI: Kuolewa siyo ishara ya mapenzi pia siyo lazima ila mpaka niamue, nina mtu wangu ninampenda sana naye pia ananipenda.

KILICHOMVUTIA
Dada nini kilikuvutia kwenye ulingo wa filamu na ukajikuta nawe umeingia huko? Ally, Moro, 0712724088
AISHA BUI: Nilikuwa navutiwa sana na muvi za nje ya nchi na nilikuwa napenda kuigiza tangu nikiwa mtoto.

NDOA
Ninavyokujua dada Aisha ni dada ambaye uko serious na kazi yako, usiyependa kujihusisha na vitendo vichafu, unajiheshimu pia huyo mtoto uliyenaye ni udanganyifu tu kwamba nitakuoa hatimaye hupotelea mitini, mimi ninavyojua unapenda kuwa kwenye ndoa na siyo vinginevyo, kaza buti dada jitahidi ingia kwenye ndoa. Rich, Dar, 0714868843

AISHA BUI: Wala siyo udanganyifu niliona bora nizae maana umri unaenda ndoa bado sijaamua na mtoto ni muhimu zaidi.
KABILA
Hivi dada Aisha wewe ni kabila gani? Diana, Dar, 0717402789
AISHA BUI: Mwarabu.

CHANGAMOTO
Aisha wewe ni msanii mkongwe wa filamu ni changamoto gani uliyowahi kukutana nayo na hautaisahau? Rachel, Mbeya, 0766120552
AISHA BUI: Sitasahau nilivyozushiwa kwamba nilikamatwa na dawa za kulevya.

KUCHUKULIANA MABWANA
Wewe ni msanii mkongwe wa filamu, eti ni kweli ninyi wasanii wa kike hampendani, kisa kuchukuliana mabwana? John Ipembe, Shinyanga, 0759918465

AISHA BUI: Mimi sipo katika hilo kundi kwa sababu hata watu wangu ninaokuwa nao hawapo huko na tambua kwamba siyo hawapendani kutokana na hilo tu bali hata mtu akiona mwenzake anamzidi kwa kitu fulani anamchukia bila sababu.
HUYU ANAMFAHAMU
Aisha nakujua kitambo tangu kipindi kile una uhusiano na Samir Saleh Behan. Msomaji, Dar, 0716662234
AISHA BUI: Ni kweli lakini ni zamani sana nikiwa bado mdogo.

ANAOMBA URAFIKI
Aisha mimi nimetokea kukupenda sana ila sijui nitakupata vipi, kama hautajali naomba unitafute kwa namba yangu hii japo nikuone live tuwe hata marafiki mimi nitaridhika. Msomaji, 0756455565
AISHA BUI: Sawa nitakutafuta.

ANAMFAHAMU
Nakujua Aisha na mdogo wako Yusra na baba yenu mlitokea Mombasa mkawa hamna pa kuishi mkawa mnakaa kwa mama Najma, Temeke (Dar). Msomaji, 0782246742
AISHA BUI: Mama Najma ni shangazi yetu na tulikuja kumsalimia tu kwani sisi tulikuwa tunaishi Kariakoo maeneo ya Gerezani (Dar).

MBONA AMEPOTEA?
Dada Aisha mimi nilikuwa nakufuatilia tangu enzi za marehemu Mpakanjia kwa nini ulipotea ghafla tena nilishakusahau ulikuwa wapi na ulikuwa unafanya nini? Mama Diki, Dar, 0714378339
AISHA BUI: Nipo sema tu muda mwingi nilikuwa safari nje ya nchi ila sasa hivi nimerudi rasmi na filamu yangu ya Mshale wa Kifo ipo mitaani pia tarajia kazi zangu nyingine kibao.
MATARAJIO
Wewe ni miongoni mwa wasanii wanaojituma sana kwenye kazi, je, nini matarajio yako kwa baadaye kama mzalendo wa Tanzania? Brosco Ngeleja, Mwanza, 0755203757
AISHA BUI: Matarajio yangu ni mengi lakini siwezi kuyaweka hadharani kwa sasa nasubiri kwanza nipate mafanikio ndiyo niyaanike maana kwa sasa naweza kuibiwa mawazo yangu.

ANAMUENZI VIPI MPAKANJIA?
Napenda kujua unamuenzi vipi aliyekuwa mwandani wako marehemu Meddy Mpakanjia? Mkemimi Serungwi, 0655832775
AISHA BUI: Siwezi kumuenzi kwa sababu tulikuwa wapenzi tukaachana tu hakunioa.

KUHUSU KANUMBA
Eti inasemekana ulishawahi kutoka kimapenzi na (Steven) Kanumba, ni kweli? Msomaji, 0769795602
AISHA BUI: Hapana, sijawahi kutoka kimapenzi na msanii katika maisha yangu.

ETI ALIKUWA MPENZI WAKE?
Aisha nakujua sana uliwahi kuwa mpenzi wangu baada ya kupata bwana mwingine ukaniacha. Saidi Selemani, Dar, 0652873660
AISHA BUI: Sijawahi kuwa na mwanaume mwenye jina hilo.

No comments: