welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Monday 8 September 2014

WEMA AMKEJELI KAJALA

Stori: Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani
NGOMA nzito! Kauli ya sexy lady wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kuwa yupo tayari kumtumikia msanii mwenzake Kajala Masanja ‘K’ kwenye kampuni yake ya KAY Entertiment tena bila malipo yoyote, imetafisiriwa kuwa ni kejeli.

Sexy lady wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’
Hivi karibuni Wema alikaririwa akisema: “Nakubali kwamba Kajala anaweza kuwa na maisha mazuri ya kiasi hicho na akanifanya mfanyakazi wake katika kamusi yake kwa sababu sioni cha kumfanya ashindwe kuwa hivyo, naamini anaweza kuniajiri na wala sina kipingamizi! hahahaa!”Msanii wa Bongo Movie Kajala Masanja ‘K’.
Baada ya kauli hiyo ya Wema, mashabiki wake waliikataa kwa maelezo kuwa alilenga kumkejeli Kajala ambaye awali aliwahi kumwajiri kwenye kampuni yake ya Endless Fame Production.

No comments: