Diamond ambaye ameweka rekodi nchini kwa kuwa msanii pekee kuchukua
tuzo tatu kwa mpigo huku tuzo hizo zikiwa ni pamoja na ya Mwanamuziki
Bora wa Kiume Afrika Mashariki, Video Bora ya Muziki wa Afro Pop,
Mwanamuziki Bora Anayechipukia hivyo alikosa tuzo moja tu ya Video Bora
kwa mwaka.
DAVIDO
“Tanzania imesimama! Diamond Platnumz ameweza tena!” aliandika
mwanamuziki huyu wa Nigeria kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.
EMMANUEL ELIBARIKI ‘NAY WA MITEGO’
“Diamond anatakiwa kuwa muwazi kwa sisi wenzake ili tuweze kuleta
tuzo nyingi Bongo. Atoe mianya kwa wasanii wenzake kwa kuwaonesha njia
kwani Nigeria wasanii wake walifanikiwa kutokana na mmoja wao
alipofanikiwa aliwaonesha njia ya kujipenyeza kimataifa zaidi.”
“Kweli Diamond anastahili kwa sababu anajituma na anafanya vizuri,
nampa hongera sana, aongeze bidii zaidi asibweteke kwa tuzo
alizopata.”WAJE
“Waooh! Hongera mkaka kwa tuzo tatu.” Aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.
“Diamond anastahili kwa kweli, wewe ni zawadi yetu, sasa hivi neno
Bongo Fleva linatajwa Afrika nzima hakutakuwa tena na maswali mengi
ukisema unatoka Tanzania, hongera sana.”
Katika kuwapa shukrani mashabiki wake kwa kumfanikisha kushinda tuzo
hizo, Diamond atatinga nazo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar
Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar ambapo pia usiku huo atapiga
shoo ya nguvu.
No comments:
Post a Comment