Chanzo
cha vurugu hizo kinadaiwa kuwa ni kukatwa mkono kwa mkulima mmoja
aishiye Kijiji cha Mketeni wilayani Kiloasa wakati akibishana na mfugaji
ambaye ni kabila la Kimasai kuhusu eneo la kulishia mifugo.
Kufuatia
kitendo hicho cha kukatwa mkono, mkulima huyo aliwafuata wenzake na
kuwapa taarifa ambapo walikusanyika na kuanzisha vurugu dhidi ya
wafugaji wa eneo hilo.Baada ya kuona kuwa bado haitoshi na baadhi ya
wafugaji kukimbia, wakulima walimalizia hasira zao katika Barabara ya
Morogoro - Dodoma ambapo waliamua kuifunga kwa takribani masaa mawili
huku wakichoma matairi.
No comments:
Post a Comment