Aliyekuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Abbas Mtemvu.
HAIJAKAA sawasawa! Siku chache baada ya Sitti Abbas Mtemvu (25)
kujivua taji la Miss Tanzania 2014 kwa madai ya kusakamwa na vyombo vya
habari kuhusu umri wake, wadau wamemwangushia uwajibikaji mwingine
wakimtaka avue mataji mengine mawili.Baadhi ya wadau wa sanaa
waliozungumza na Risasi Mchanganyiko Jumatatu iliyopita jijini Dar
walisema kama kweli Sitti ana dhamira safi ya kukwepa kusakamwa basi ni
bora kwake akavua na mataji ya Miss Chang’ombe na Miss Temeke ambayo
ndiyo yaliyompa tiketi ya kwenda kambi ya Miss Tanzania na kushinda.
Wadau hao walisema kuwa, sheria za Miss Tanzania zinaanzia
vitongojini, wilaya, mikoa, kanda na hatimaye taifa kwa hiyo kama skendo
ya kudanganya umri imemla mpaka akaamua kujisalimisha, basi bado hana
sifa za kuwa Miss Chang’ombe na Miss Temeke wa mwaka 2014.
“Kwanza kabisa nasema Sitti hajavua taji la Miss Tanzania kwa sababu
ya kusakamwa na vyombo vya habari kuhusu kudanganya umri bali ni kweli
amedanganya, anajijua.
“Kama angekuwa hajadanganya, kwa nini asitoe paspoti yake
inayomwonesha ana umri wa miaka 23? Mambo yalimfika shingoni ndiyo
maana. Anachotakiwa ni kuvua taji la Miss Chang’ombe na Miss Temeke
mwaka huu,” alisema Ismail Chandu, mkazi wa Temeke jijini Dar.
Shindano la kumsaka Miss Chang’ombe lilifanyika Juni 27, mwaka huu
kwenye Ukumbi wa TCC Chang’ombe, Dar ambapo Sitti aliibuka kidedea
akifuatiwa na Paulina Elisante (anayetakiwa kuchukua taji), wa tatu ni
Derena David.
Shindano la Miss Temeke 2014 lilifanyika Agosti 22, mwaka huu kwenye
Ukumbi wa TCC Club, Chang’ombe jijini Dar ambapo Sitti Mtemvu aliibuka
kidedea akifuatiwa na Salama Saleh (anayetakiwa kushika nafasi ya
kwanza) na nafasi ya tatu ilitwaliwa na Neema Mollely.
Novemba 5, mwaka huu, Sitti Mtemvu aliiandikia barua Kamati ya Miss
Tanzania inayoongozwa na Hashim Lundenga akisema ameamua kwa hiyari yake
kuvua taji hilo.Sitti alifikia uamuzi huo baada ya kuandamwa na skendo
ya kudanganya umri wakati akigombea taji hilo.
No comments:
Post a Comment