ACHANA na
mazingira ya kifo cha Bilionea maarufu wa Bukoba, Leonard Mtensa
aliyefariki saa chache baada ya kufanya mapenzi ndani ya gari kuacha
gumzo, gumzo lingine lilitokea wakati wa mazishi yake ambayo
yalihudhuriwa na wananchi wengi kutoka ndani na nje ya mkoa, mkanda
kamili huu hapa.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia mazishi hayo mwanzo mwisho,
msiba huo ulikuwa wa pekee kwani haijawahi kutokea kwa yeyote kuzikwa na
umati mkubwa kiasi hicho na kusababisha watu wote wasimame kiasi cha
kuwafanya askari wa usalama barabarani kufanya kazi ya ziada kuhakikisha
mambo yanakwenda sawa.
Wananchi
wakiwa barabarani kushuhudia msafara huo ukipita. “Msafara ulianzia
mochwari ya Hospitali ya Bukoba, ukapita katika klabu yake ya Lina’s
kisha ukapitia mtaa wa Jamhuri lilipo Soko Kuu la Bukoba kisha kuelekea
kijiji cha Kyaikailabwa.
“Ilikuwa si mchezo, hii ni historia kwa Bukoba. Haijawahi kutokea
msiba wa mtu wa kawaida ukawasababisha watu kujipanga barabarani,
trafiki kuongoza harakati utafikiri mapokezi ya rais,” kilisema chanzo.
Inadaiwa kuwa msafara wa magari ulivunja rekodi kwani wakati magari
mengine yalikuwa yameshafika makaburini, mengine yalikuwa bado kwenye
foleni nyumbani.
Jeneza likibebwa kuelekea makabulini.
Chanzo hicho kilizidi kupasha habari kuwa, msafara wa kutoka nyumbani
kwa marehemu, Bukoba mjini hadi katika Kijiji cha Kyaikalabwa ambacho
kipo umbali wa kilomita 3, ulikuwa mrefu kiasi ambacho magari
yalijipanga kuanzia mjini hadi kaburini.
“Palifunga kabisa, huwezi amini ule msururu wa magari ulianzia Bukoba
mjini hadi Kyaikailabwa, magari yenyewe asilimia kubwa yalikuwa ya
maana.“Marehemu alikuwa tajiri na baadhi ya marafiki zake pia walikuwa
matajiri sasa ilikuwa ni balaa maana magari ya kifahari tupu yalipamba
msafara huo.
Mwili wa marehemu ukiandaliwa kwa ajili ya mazishi. VIGOGO NJE YA NCHI
“Mbali na matajiri na wafanyabiashara wazawa kuhudhuria msiba huo,
walikuwepo marafiki wengi wa marehemu kutoka Afrika Mashariki na Kati
ambao kwa namna moja au nyingine walikuwa wakimfahamu marehemu kwa
kushirikiana nao kibiashara,” kilisema chanzo chetu. WAKATOLIKI WAKATAA
KUMZIKA
Chanzo hicho makini kilidai kuwa, kutokana na mazingira ya kifo na
watu waliokwenda kuomba misa ya msiba huo kutokidhi vigezo, viongozi wa
kanisa katoliki walikataa kuongoza ibada ya mazishi.
Ilidaiwa kuwa waliokwenda kuomba misa hiyo hawakuwa na sifa za
kiimani (hawakuwa wakatoliki) sambamba na kutotumia busara wakati wa
kujieleza.
Ndugu
wa marehemu wakilia kwa uchungu. “Waliokwenda kuomba misa hawakuwa
wakatoliki halafu mbaya zaidi hawakuwa na busara wakati wa kujieleza,
mapadri wakawagomea kuongoza ibada hiyo,” kilisema chanzo.
Badala yake, inadaiwa kuwa ibada ya kumuombea marehemu iliendeshwa na wakristo wa Kilokole iliyofanyika nyumbani kwake.
TUJIKUMBUSHE
Marehemu Mtensa aliyeacha mjane na watoto kwa mkewe wa ndoa, alikutwa
na umauti Novemba 18, mwaka huu saa chache baada ya kuzidiwa akiwa
ndani ya gari lake akifanya mapenzi na mchepuko wake aliyejulikana kwa
jina la Jackline Hassan.
Mwili
wa marehemu ukiingizwa kaburini. Kitendawili kingine kilichoteguliwa ni
kuhusu msichana Jack, mwenye umri wa miaka 25, ambaye awali iliaminika
kuwa ni mpenzi wake aliyekutana naye ghafla tu, lakini inasemekana
alikuwa ni mpenzi wa muda mrefu wa Mtensa na kwamba hata wakati flani
alipokuwa akienda Uganda kuwaangalia watoto wake waliokuwa wakisoma
huko, alikuwa akiongozana naye.
Aidha, stori nyingine kutoka huko zinadai kwamba polisi wamekuwa
wakitaka kumuachia msichana huyo wakiamini hakuwa na kosa, ingawa hakuna
taarifa zozote zilizokwishatolewa hadi sasa kuhusu uchunguzi
waliofanya.
No comments:
Post a Comment