UPEPO
mbaya unaendelea kuvuma ndani ya Klabu ya Bongo Movie Unity! Safari hii
umewakumba mastaa wakubwa klabuni hapo, Devotha Mbaga, Aunt Ezekiel na
Jennifer Kyaka ‘Odama’ ambao wanadaiwa kutimuliwa kundini kwa sababu ya
kujiweka karibu na mwenyekiti wa klabu hiyo aliyejiuzulu, Steven Mengere
‘Steve Nyerere’.
“Wamewaengua baadhi ya wasanii ambao wameona hawana sifa ya kubaki
kundini, miongoni mwao ni Devotha, Aunt na Odama. Wamesema wanahitaji
mastaa wenye msimamo siyo kujipendekeza upande wa Steve, siku si nyingi
watayaanika majina ya wenye sifa za kubaki kundini,” kilisema chanzo
hicho.
Staa
wa filamu bongo Devota Mbaga. Chanzo hicho kilizidi kumwaga ‘ubuyu’
kuwa, wasanii walioenguliwa ni wanachama hai lakini si wanachama wenye
msimamo na baadhi yao wameonesha udhaifu wa kuwa karibu na Steve Nyerere
ambaye sasa anafanya harakati zake peke yake.
Baada ya habari hizo kutua katika rada ya Ijumaa, mapaparazi wetu
waliwaendea hewani mastaa hao wakubwa waliodaiwa kufukuzwa, mambo
yalikuwa hivi:
Mkali
wa filamu Bongo, Jennifer Kyaka 'Odama'. Devotha: Mimi ndiyo kwanza
nakusikia wewe siku zote nipo nyumbani sijui hata habari za kikao hicho
na sielewi wameniengua vipi wakati mimi ni mwanachama hai na ni miongoni
mwa waanzilishi toka tulipokuwa watu saba, lakini kama wameamua hivyo
sawa kwani siyo kwamba ukitoka ndiyo mwisho wa maisha.
Odama: Hakuna kitu kama hicho, wanaoenguliwa ni viongozi siyo
wanachama, watanienguaje bila kunipa taarifa? Kwanza ndiyo nasikia sijui
chochote ndiyo napata taarifa kutoka kwako.
Kwa upande wa Aunt Ezekiel, simu yake iliita bila kupokelewa.
No comments:
Post a Comment