Kwa
mujibu wa ‘shujaa’ wetu, tukio hilo la aibu ya aina yake lilijiri
juzikati kwenye Ukumbi wa Savoy mjini hapa ambapo wanawake hao
walialikwa kuburudisha kwenye sherehe ya harusi ya jirani yao. Mtu mzima
ovyoo! Akina mama watatu ambao ni wake za watu, wanaounda Kundi la
Heshima Pesa Shikamoo Makelele lenye maskani yake maeneo ya Mawenzi
mjini hapa wanadaiwa kuwachefua baadhi ya watu baada ya kujitoa fahamu
na kumwaga ‘lazi’ hadharani na mbaya zaidi mbele ya watoto wadogo.
Wanawake
hao waliofahamika kwa majina ya watoto wao ni pamoja na mama Sabra
aliyekuwa akibinuka, aliyevalia kigauni kifupi cha draftidrafti.Mwingine
alikuwa ni mama Jenifa aliyekuwa ametupia kimini cha njano na mama
Athuman ambao kwa pamoja walikuwa na vikuku miguuni.Mama Sabra mwenye kigauni kifupi cha draftidrafti, mama Jenifa wakimwaga radhi ukumbini.
Mtu wetu
huyo aliyekuwa ndani ya ukumbi huo aliwashuhudia wanawake hao wakimwaga
lazi mara baada ya MC kuita kundi lao kwa ajili ya kutoa zawadi.Mama Sabra akijiachia kwa raha zake bila kujali matokeo.
Kabla ya
kutoa zawadi, wamama hao walimfuata DJ na kumtaka kuwawekea wimbo wowote
wa Taarab, wakawekewa ambapo wakiwa na zawadi yao ya doti moja ya
khanga, walipita mbele ya maharusi kwa mbwembwe zote na baada ya
kukabidhi zawadi hiyo ndipo balaa lilipoanza.Mama
Sabra akizidi kumwaga radhi bila uoga. Huku wakipeana nafasi na mara
nyingine kulaliana, walikuwa wakijibinua na kuonesha staili za chumbani
huku ‘makufuli’ yakiwa nje, jambo lililotibua harusi hiyo.
No comments:
Post a Comment