Rais wa TFF, Jamal Malinzi
Kikao
cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kimefanyika leo kujadili matukio ya hivi karibuni, hasa
mwenendo wa wadau wa Bodi ya Ligi. Shirikisho linatoa tamko kwa umma
kama ifuatavyo:
- Kamati ya Utendaaji imesikitishwa na taarifa za upotoshaji kuhusu kanuni mpya za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), hivyo inaomba radhi kwa wadau ambao wameguswa na kusumbuliwa na matukio hayo.
2.Kufuatia
matukio hayo, Sekretarieti ya TFF kwa niaba ya Kamati ya Utendaji,
imefungua mashtaka kwenye Kamati ya Nidhamu dhidi ya Dk. Damas Ndumbaro
ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Ligi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya
Klabu ya Simba. Pia wadau wote waliohusika na upotoshaji huo wakiwemo
wafanyakazi wa TFF na Bodi ya Ligi watashughulikiwa kulingana na nafasi
zao.
3.Kutokana
na madai ya klabu kuhusu vipengele kadhaa vya Kanuni za Ligi Kuu
2014/15, Kamati ya Utendaji imepanga kukutana na viongozi wa klabu za
Ligi Kuu siku ya Jumamosi, Oktoba 18 mwaka huu ili kuwasikiliza na
kushauriana kuhusu changamoto za kikanuni na uendeshaji wa mashindano
kwa ujumla.
4.Kamati
ya Utendaji itaendelea kuboresha Kanuni za Uendeshaji Bodi ya Ligi
(Governing Regulations) ili kuweka uwiano wa utendaji na kuepusha
tofauti kati ya Bodi ya Ligi, vilabu na TFF. Aidha Kamati ya Utendaji
itafanya kila linalowezekana kuboresha ligi kwa kuijengea uwezo Bodi ya
Ligi kwa lengo la kuwa na ligi zinazoendeshwa kisasa (Professional
Leagues).
No comments:
Post a Comment