Kijana
mmoja mkazi wa Kimandolu jijini Arusha, (jina kapuni) mwenye umri wa
miaka 18 amelazwa katika hospitali ya mkoa Mount Meru baada ya kubakwa
na kisha kukatwa ulimi na mwanamke mmoja aliyekuwa akimtaka kimapenzi.
Tukio
hilo la kusikitisha limetokea juzi majira ya saa 6.30 usiku katika eneo
la Tindigani, kimandolu, wakati mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina
moja la mama Abuu alipofika katika bar hiyo kama mteja na baadaye
alimlazimisha mhudumu wa bar hiyo ambaye ni majeruhi kufanya mapenzi
bila ridhaa yake.
Akiongea
na mwandishi wa habari hii mfanyakazi katika bar hiyo, inayomilikiwa na
mwenyekiti wa mtaa ,Joel Mbasha alisema mnamo majira ya usiku alikuja
mwanamke huyo na kuagiza kinywaji huku yeye akimhudumia kabla
hajamgeuzia kibao.
Alieleza
kuwa ilipotimu majira ya saa 6.30 wateja waliisha katika bar hiyo na
kuamua kufunga bar ,hata hivyo mwanamke huyo ndiye aliyebaki pekee
akinywa pombe taratibu katika eneo hilo ndipo alipomlazimisha kufanya
kitendo hicho ambapo alimziba mdomo kwa kutumia kinywa chake na baadae
alifanikiwa kumng’ata ulimi na kuutema chini.
Majeruhi
huyo kwa sasa hali yake bado mbaya kwani hawezi kuongea na muda mwingi
anatokwa na damu nyingi hatua ambayo imewalazimu wahudumu katika
hospitali hiyo kumwekea ndoo ya kutemea damu.
Jeshi la
polisi mkoani Arusha limethibitisha tukio hilo na kwamba mtuhumiwa
anashikiliwa na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani
No comments:
Post a Comment