Leo
ndo siku ambayo aliyekua msanii wa kundi la Wanaume Family ‘YP’
amezikwa ikiwa imepita siku moja tu tangu afariki dunia. Chanzo cha kifo
cha msanii huyo ni ugonjwa wa kifua ambao ulikua ukimsumbua kwa mda
mrefu. Bongoclan imepata nafasi ya kufanya mahojiano na Juma Nature
ambapo alisema ni huzuni kubwa sana kumpoteza msanii mwenzake ambaye
walikua wakifanya kazi pamoja tangu zamani.
Pia tuliweza kumuuliza
ni kitu gani anajivunia kuhusu mziki wake na alikua na haya ya kusema ”
Mimi najivunia nina mashabiki wengi kuliko mtu yeyote Tanzania, nina
mashabiki wengi sana ambao hawana fitna na sio wa kutengenezwa.
Wanaotengeneza mashabiki huo ni ulimbukeni kwa sababu labda ni tamaaa za
pesa, kuna mtu mwingine anataka kutengeneza kitu labda anataka kua mtu
flani kwa kuforce. Mziki tuliokua tunafanya sisi sio wa kutengeneza kama
mtu anaomba nyimbo yako redion anaomba sio kwamba msanii kamwambia piga
simu uombe nyimbo yangu redion. Sasa athari zake tutakosa msanii bora
ambaye ataiwakilisha Tanzania au hata Afrka.
No comments:
Post a Comment