Ali Akbar Salehi Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
yuko mjini Geneva, Uswisi kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa
Baraza la Haki za Binadamu na Kongamano la Upokonyaji Silaha. Salehi
amebainisha katika hotuba aliyoita jana usiku katika mkutano huo wa
Geneva mitazamo ya Iran kuhusu masuala tofauti likiwemo suala la haki za
binadamu na upokonyaji silaha. Mkutano huo unafanyika katika hali
ambayo, kuwepo vichwa 27 elfu vya silaha za nyuklia ambapo sehemu kubwa
ya silaha hizo zinamilikiwa na Marekani na nchi nyinginezo,
kunahesabiwa
kuwa tishio kubwa kwa usalama wa dunia. Hata hivyo usalama wa nyuklia
haumaanishi kuwa mataifa yazuiwe haki yao ya kisheria ya kustafidi na
teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani. Marekani na nchi kadhaa
duniani kwa kutumia uongo na madai yasiyo na msingi zinataka kuyaamulia
mataifa mengine mustakbali wao, na kutumia Baraza la Usalama kama wenzo
wa kupasisha maazimio ya kisiasa na ya kidhulma ili kudhamini maslahi
yao haramu duniani. Kuhusu kadhia ya haki za binadamu pia kuna wasiwasi
unaofanana na huo. Hii ni kwa sababu Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya
zinazodai kuwa ni watetezi wa haki za binadamu, zimegeuza Umoja wa
Mataifa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuwa wenzo wa
kisiasa wa kufikia malengo yao ya kikoloni. Hii ni katika hali ambayo
fikra za walio wengi duniani zinatambua vyema nafasi ya wazi ya Marekani
katika kusambaza silaha za nyuklia, na ulimwengu mzima unajua kwamba
Marekani ni nchi pekee duniani iliyowahi kutumia bomu la nyuklia dhidi
ya raia wasio na hatia. Pia Israel imetengeneza maghala ya silaha za
nyuklia kwa msaada wa serikali ya Washington. Marekani vilevile
inashirikiana kwa kiasi kikubwa katika uwanja wa nyuklia na nchi ambazo
hazijatia saini Mkataba wa Kuzuia Kuzalisha na Kusambaza Silaha za
Atomiki N.P.T. Hii ni katika hali ambayo kwa mujibu wa sheria za Wakala
wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki na Mkataba wa N.P.T, nchi zenye
teknolojia ya nyuklia zinapaswa kusaidia mipango ya nyuklia ya amani ya
nchi wanachama wa Mkataba wa N.P.T na hazipaswi kushirikiana na nchi
ambazo si wanachama. Ukweli ni kuwa, Marekani ambayo kwa mujibu wa
baadhi ya ripoti ina karibu vichwa vya nyuklia elfu 10 na ni mkiukaji
mkubwa wa mikataba ya kimataifa, inatumia vibaya Baraza la Usalama na
Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia IAEA kama njia ya kuziwekea
mashinikizo nchi nyinginezo. Pia inadai kwamba Iran inakusudia
kutengeneza bomu la atomiki kwa kutoa madai ya uongo na yasiyo na msingo
wowote. Ni wazi kuwa madai ya Marekani na baadhi ya washirika wake
wachache yanayotolewa dhidi ya Iran ni sehemu ya malengo ya kisiasa na
kipropaganda ya nchi za Magharibi, yenye azma ya kuwapotosha waliwengu
kuhusu tishio halisi la amani na usalama linalotokana na kuwepo silaha
za nyuklia duniani. Kwa kuzingatia kweli huo inatarajiwa kuwa, Mkutano
wa Haki za Binadamu na Kongamano la Upokonyaji Silaha ambao ulianza
Jumatatu mjini Geneva na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran,
itakuwa fursa nzuri ya kubainishwa ukweli huo.
No comments:
Post a Comment