PAMOJA na kutumia nguvu nyingi kukanusha kwenye mitandao kwamba ndoa yao haijavunjika, mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Habash ‘G. Habash’ na ‘mtalaka’ wake, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’, Jumamosi iliyopita walifanya tukio lililowashangaza watu kufuatia kila mmoja kuingia ukumbini akiwa na kampani yake na kukwepana kama paka na panya, Amani liliwanasa kwa vile lilikuwepo.
Mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Habash ‘G. Habash’ akiwa na Miss Mara 2000, Rashida Wanjara.
Tukio hilo lililoamsha minong’ono kwa watu waliosoma mchezo mzima, liliibukia ndani ya Ukumbi wa Ten Lounge (zamani Business Park) uliopo Makumbusho, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na uzinduzi wa albamu ya Bongo Fleva.
WALIVYOKAA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Gardner alipoingia alikwenda kukaa kwenye meza na watu wengine watatu, baadaye akafika Miss Mara 2000, Rashida Wanjara na kuunga ambapo walikuwa wakibadilishana mawazo na kufunguliana vinywaji kwa meno na kumiminiana kwenye glasi.
JIDE NAYE
Wakati Gardner ambaye pia hujulikana kwa jina la utani la Kapteni akiendelea kujipoza na Rashida na wengine, Jide yeye alikaa meza moja na kijana mmoja aliyevalia shati la kitenge la mtindo uliowahi kutamba miaka mitano nyuma, wengine huita Mackezie sanjari na wadada wawili.
WALICHOTAKA WATU
Baadhi ya watu walisikika wakishauri kwa sauti ushauri ambao haukuwafikia wawili hao ambapo walisema kama kweli ndoa hiyo haijavunjika, ni vyema Jide angeenda kwenye meza aliyokaa Gardner na kusema chochote kisha kuondoka hali ambayo hakuwepo.Mtalaka’ wa Gardner, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ (kulia) akijaribu kukwepa kamera za Global.
PAKA NA PANYA!Baadhi ya watu walisikika wakishauri kwa sauti ushauri ambao haukuwafikia wawili hao ambapo walisema kama kweli ndoa hiyo haijavunjika, ni vyema Jide angeenda kwenye meza aliyokaa Gardner na kusema chochote kisha kuondoka hali ambayo hakuwepo.Mtalaka’ wa Gardner, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ (kulia) akijaribu kukwepa kamera za Global.
Mtu mmoja aliyekuwa amehudhuria shughuli hiyo na mkewe, alimuita paparazi wetu na kumuuliza: “Kwani, Jide na Gardner sasa ni paka na panya?”
Mwandishi: “Kivipi?”
Mtu: “Namwona Jide yuko na kampani yake, Gardner naye na kampani yake kule. Unajua paka na panya ni vigumu kukutana! Hawa kweli hawapo sawasawa,” alisema mtu huyo alijitambulisha kwa jina la Yahya.
Akaendelea: “Unajua ninavyojua mimi, Gardner ni kijana mpole sana, mwenye upendo, ila Jide ni mkali. Halafu kwa sababu yeye Jide ana pesa naamini alitaka kumpandia kichwani mumewe wakati anajua yeye ni kichwa cha nyumba. Pesa na ndoa mambo mawili tofauti.”
WAWINDWA NA KAMERA
Muda mwingi paparazi wetu aliwavizia Gardner na Rashida na kufanikiwa kuwafotoa picha kadhaa lakini kimbembe kilikuwa kwa Jide ambaye alionekana kuwa makini na kukwepa kamera ya paparazi wetu mara kadhaa huku akionekana kuwa na hasira na kuna muda meza yake iliparaganyika baada ya mwanga wa kamera kuwamulika yeye na kampani yake.
ANGALIA HII
Katika hali iliyodhihirisha wawili hao hawako sawasawa, muda f’lani Gardner aliinuka na kuelekea upande aliokaa Jide ambapo mwanamuziki huyo naye alionekana kama kutaka kukimbia na kumfanya Gardner kubadili mwelekeo wa safari yake.Gardner akiendelea kufatilia jambo.
KUNA HII PIAKatika hali iliyodhihirisha wawili hao hawako sawasawa, muda f’lani Gardner aliinuka na kuelekea upande aliokaa Jide ambapo mwanamuziki huyo naye alionekana kama kutaka kukimbia na kumfanya Gardner kubadili mwelekeo wa safari yake.Gardner akiendelea kufatilia jambo.
Mmoja wa mashuhuda aliyekuwa ukumbini hapo naye alimwambia paparazi wetu kuwa, aliwaona wawili hao wakikwepana baada ya kukutana kwenye njia ya kuelekea maliwatoni.
GARDNER AZUNGUMZA NA AMANI
Juzi, Amani lilimtafuta Gardner kwa njia ya simu na kumuuliza ni kwanini yeye na Jide kila mmoja aliingia ukumbini na kampani yake.Gardner: “Kaka, yeye (Jide) alikwenda pale kumpa tafu yule aliyekuwa akizindua albamu yake pale. Sasa isingekuwa rahisi tugandane pamoja kila wakati. Lakini hayo unayoniambia ni madai tu.”
TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni, ndoa ya wawili hao iliripotiwa kuvunjika na kila mmoja kushika njia yake huku Gardner akiwa anakanusha mara kwa mara kwamba ndoa ipo imara. Jide naye amekuwa akiweka kwenye mtandao wa Instagram picha yake yenye kidole cha pete ya ndoa bila maelezo!! Ni shiida!
No comments:
Post a Comment