welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday, 31 December 2014

WAGOMBANAO NDIO WAPATANAO MR NICE NA DUDU BAYA WAMALIZA TOFAUTI ZAO


Wasanii wa muziki waliowahi kuwa mahasimu, Dudu Baya na Mr Nice wamemaliza tofauti zao na kuanza kufanya tour yao ya muziki iliyoanzia Moshi.

Akizungumza kutoka Moshi akiwa na Dudubaya, Mr Nice alisema wameamua kumaliza tofauti zao na kuanza kufanya kazi pamoja.
“Kesho tuna show halafu tuna show tena Namanga mpakani mwa Tanzania Kenya, huyu ni swahiba yangu, ninampa shavu kwa sababu huku ni kwangu, na sina ubaya naye mambo freshi, yale yalishaisha sisi ni marafiki na ni ndugu,” Mr Nice ameiambia Bongo5.
Kwa upande wake Dudu Baya amesema amefurahishwa kuwa pamoja na Mr Nice na kuanza kazi za kutafuta pesa wakiwa pamoja huku akitania kuwa ‘Mamba amekutana na Kenge’.
Dudubaya aliwahi kumvamia Mr Nice akiwa stejini na kumjeruhi kwa kipigo kikali

No comments: