welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday, 10 December 2014

AMANDA WA BONGO MOVIE ANASWA NA KIJEBA CHA KIZUNGU


Msanii nyota wa filamu Tanzania, Tamrina Poshi maarufu kama Amanda akiwa na mzungu.MSANII nyota wa filamu Tanzania, Tamrina Poshi maarufu kama Amanda, amenaswa katika picha akiwa na mzungu anayeonekana kumzidi umri ambaye unaweza kumwita kijeba aliyemtambulisha kama rafiki yake. Habari kutoka chanzo cha kuaminika zinasema, picha hizo ziliibwa katika simu ya msanii huyo na mtu asiyefahamika, ambaye kwa lengo lisiloeleweka, alianza kuzitawanya kwa watu mbalimbali. 
Inadaiwa kuwa Amanda amekuwa akionekana sehemu tofauti tofauti jijini Dar akiwa na mzungu huyo ambaye anasemekana kuwa na makazi yake maeneo ya Masaki.
Amanda alionekana kushtushwa baada ya kuulizwa kuhusu kuwepo kwa picha hizo na kukiri kuwa ni kweli mtu huyo anafahamiana naye.
Tamrina Poshi maarufu kama Amanda akipozi.“Duh! hizo picha zimefikaje kwenu? Jamani haya ni maisha yangu binafsi naombeni mniache na huyo jamaa ni rafiki yangu sana, kwanza siyo mtanzania ni raia wa Uturuki,” alisema muigizaji huyo.

No comments: