welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday, 12 November 2014

DUNIA IMEKWISHA JAMANI...WAKE ZA WATU WAMWAGA RADHI HADHARANI BILA AIBU HUKO MOROGORO!

Wake za watu wanaofahamika kama mama Sabra mwenye kigauni kifupi cha draftidrafti, mama Jenifa mwenye kimini cha njano na mama Athuman wakijitoa ufahamu mbele ya mahrusi.
Kwa mujibu wa ‘shujaa’ wetu, tukio hilo la aibu ya aina yake lilijiri juzikati kwenye Ukumbi wa Savoy mjini hapa ambapo wanawake hao walialikwa kuburudisha kwenye sherehe ya harusi ya jirani yao. Mtu mzima ovyoo! Akina mama watatu ambao ni wake za watu, wanaounda Kundi la Heshima Pesa Shikamoo Makelele lenye maskani yake maeneo ya Mawenzi mjini hapa wanadaiwa kuwachefua baadhi ya watu baada ya kujitoa fahamu na kumwaga ‘lazi’ hadharani na mbaya zaidi mbele ya watoto wadogo. 
Wanawake hao waliofahamika kwa majina ya watoto wao ni pamoja na mama Sabra aliyekuwa akibinuka, aliyevalia kigauni kifupi cha draftidrafti.Mwingine alikuwa ni mama Jenifa aliyekuwa ametupia kimini cha njano na mama Athuman ambao kwa pamoja walikuwa na vikuku miguuni.Mama Sabra mwenye kigauni kifupi cha draftidrafti, mama Jenifa wakimwaga radhi ukumbini.
Mtu wetu huyo aliyekuwa ndani ya ukumbi huo aliwashuhudia wanawake hao wakimwaga lazi mara baada ya MC kuita kundi lao kwa ajili ya kutoa zawadi.Mama Sabra akijiachia kwa raha zake bila kujali matokeo.
Kabla ya kutoa zawadi, wamama hao walimfuata DJ na kumtaka kuwawekea wimbo wowote wa Taarab, wakawekewa ambapo wakiwa na zawadi yao ya doti moja ya khanga, walipita mbele ya maharusi kwa mbwembwe zote na baada ya kukabidhi zawadi hiyo ndipo balaa lilipoanza.Mama Sabra akizidi kumwaga radhi bila uoga. Huku wakipeana nafasi na mara nyingine kulaliana, walikuwa wakijibinua na kuonesha staili za chumbani huku ‘makufuli’ yakiwa nje, jambo lililotibua harusi hiyo.

No comments: