welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Friday 14 November 2014

DIVA NIWAPO CHUMBANI NI MWENDO WA NGUO LAINII!


Mkali katika tasnia ya filamu bongo, Halima Yahaya 'Davina'.
Leo kwenye safu yetu hii tunaye mwanadada kutoka kwenye tasnia ya filamu Bongo anayefahamika kwa jina la Davina lakini jina alilopewa na wazazi wake ni Halima Yahaya.
Kama ilivyo ada naye anajibu maswali 10 yahusuyo maisha yake binafsi na kisanii ambayo paparazi wetu Hamida Hassan alimbana na aliyajibu kama ifuatavyo;
Ijumaa: Najua una dada wa kazi, unapokuwa nyumbani huwa unafanya nini?
Davina: Licha ya kuwa na dada wa kazi, nikiwa nyumbani si mtu wa kukaa tu, napenda kufanya usafi wa nyumba yangu, kupika na kucheza na mtoto.
Ijumaa: Je, ni chakula gani unachopendelea kumpikia mumeo?
Davina: Kiukweli mume wangu anapenda sana makaroni na nyama ya kusaga, ili kumfanya awe na furaha huwa nampikia chakula hicho.
Ijumaa: Ni sehemu gani ya mwili wako unayoipenda zaidi?
Davina: Sibagui, kila sehemu ya mwili wangu naipenda na namshukuru Mungu kwa kuniumba hivi nilivyo.
Ijumaa: Uwapo chumbani na mumeo, nguo gani ambazo unapendelea kumvalia?
Davina: Hahaha, niwapo eneo hilo navaa nguo lainiii na vipensi ndiyo usiseme!
Ijumaa: Kiufupi wewe ni mrembo, unamvutia kila mwanaume, unajilinda vipi na vishawishi vya wanaume wakware?
Davina: Namshukuru Mungu kwa kunipa ndoa kwani ndiyo inanifanya naweza kuepuka vishawishi. Najiheshimu na kuiheshimu ndoa yangu.
Ijumaa: Ikitokea umebaini mumeo kakusaliti utachukua uamuzi gani?
Davina: Kwanza ni kitu ambacho sikitarajii kabisa kutokana na mapenzi anayonionesha na uaminifu alionao.
Davina akipozi.
Ijumaa: Kwa nini hivi sasa umekuwa ukiigiza sana sehemu ya mama tofauti na ilivyokuwa huko nyuma?
Davina: Unajua hivi sasa mimi ni mama, kwahiyo ninapoigiza nafasi hiyo huwa navaa uhusika ipasavyo. Hata hivyo, nafasi nyingine pia huwa nafanya vizuri.
Ijumaa: Umejaaliwa kupata mtoto mmoja, je una mpango wa kuongeza mwingine na je unatarajia kuwa na familia ya watoto wangapi?
Davina: Siwezi kusema nahitaji familia ya watoto wangapi ila Mungu atakaonijaalia. Kwa sasa sina mpango wa kuongeza mwingine mpaka baadaye sana.
Ijumaa: Wewe umeolewa, unawazungumziaje wasanii wenzako ambao wana watu wao lakini wanachepuka tena wakati mwingine bila kificho?
Davina: Nihimize wasanii kujiheshimu na kuziheshimu ndoa zao, kama wana wapenzi basi watulie. Hii kurukaruka hasa katika ulimwengu wa sasa ni kujitafutia matatizo katika siku zijazo.
Ijumaa: Unayazungumziaje haya mabifu ndani ya Bongo Muvi?
Davina: Unajua maendeleo hayawezi kupatikana kwenye sanaa kama hatutakuwa kitu kimoja. Mabifu si kitu kizuri, mimi nasema tuna kila sababu ya kuondoa tofauti zetu.

No comments: