welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday, 15 October 2014

WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE WAWILI KUJERUHIWA BAADA YA GALI KUPINDUKA MKOANI LINDI

Na Abdulaziz Ahmed, Lindi
Watu wawili wamekufa na wawili kujeruhiwa baada ya gari waliyokuwa wanasafiria kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Michenga, wilaya ya Ruangwa Ruangwa mkoani Lindi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi, ACP Renatha Mzinga alisema gari hiyo aina ya Toyota Rava4 yenye namba za usaji T574CWC.Iliyokuwa inaendeshwa na Mohamed Mchalaganya(27) iliacha njia na kupinduka katika barabara ya Ruangwa-Nanganga, ilitokea jana saa 11.30 jioni.
Kamanda Mzinga aliwataja waliokufa kwenye ajali hiyo kuwa ni Binasa Mapua(51) mkazi wa Tabata Dar-eS-salaam na Elizabeth Chipoleka(53),mkazi wa Yombo, Dar es salaam.
Kamanda Mzinga amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Mussa Mchalanganya na Rashid Mchalanganya ambaye ni mwanafunzi katika Chuo cha Usafirishaji (NIT), ambapo wote ni wakaazi wa Tabata, Dar es salaam. Dereva wa gari hilo ametiwa mbaroni na upelelezi unaendelea kujua chanzo hasa cha ajali hio.

No comments: