welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Thursday, 9 October 2014

Wakamatwa na polisi kwa kulima shamba huku wakiwa uchi wa mnyama


Jeshi la polisi Mkoani Simiyu linawashikilia watu wanne wa familia moja kwa tuhuma ya kukutwa wakilima uchi wa mnyama shambani kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina. Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu Venansi Kimario alisema tukio hilo limetokea septemba 2 majira ya saa 12 asubuhi katika kijiji cha Bushikwamala kata ya Kalemela wilayani Busega Mkoani Simiyu. Kimario alisema kuwa watu hao walikamatwa na jeshi la polisi alfajirihuko Bushigwamhala wakiwa wanalima kwenye shamba lao na walipohojiwa walidai kuwa walielekezwa na babu yao kipindi cha uhai wake kuwa wakilima uchi watapata mavuno mengi.
Kamanda Kimario aliwataja waliokamatwa kuwa ni Makoye Kagoje (42), na mke wake Neema Kigwela (31) pamoja na watoto wao, mmoja wa kiume (15) na wa kike (12) majina yamehifadhiwa. Aidha Kimario alisema watu hao pamoja na watoto wao wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kukutwa wakifanya vitendo vya ushirikina. Babu yao alishafariki mwaka jana na aliwaambia kuwa wakilima wapo uchi watapata mavuno mengi, hivyo waliamua kufanya hivyo kutokana na wosia wa babu yao 
Alisema baada ya jeshi la polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wem aliliweza kufika katika eneo hilo na kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa wanaendelea kulima bila nguo. Hata hivyo Kimario amewataka watu wasijishirikishe kwenye vitendo vya ushirikina na siyo kwamba ukilima uchi utapata mazao mengi tofauti na kufuata kanuni za kilimo bora, viongozi wa madhehebu ya dini na viongozi wa serikali tuwaelimishe watu waachane na imani za kishikina.

No comments: